Ticker

6/recent/ticker-posts

TAMASHA LA 15 LA KIJINSIA KUFANYIKA NOVEMBA 7-10 KWENYE VIWANJA VYA TGNP

TAMASHA la 15 la Kijinsia ambalo linaratibiwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania TGNP linatarajiwa kuanza Novemba 7-10,2023 katika Viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam ambapo wadau mbalimbali wanatarajia kushiriki Tamasha hilo.

Akizungumza leo Septemba 2, 2023 jijni Dar es Salaam, katika maandalizi ya tamasha hilo, Afisa Mawasiliano wa TGNP, Monica John, amesema kuwa tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuliwa na watu zaidi ya 1500 ambao watatoka nchi mbalimbali wa hapa nchini na kutoka nje ya nchi.

"Tamasha hili litakusanya watu kutoka bara la Afrika na mabara mengine."

Amesema kuwa lengo la Tamasha hilo kujifunza pamoja na kusheherekea mafanikio katika harakati za ukombozi wa mwanamke duniani na Tanzania kwa ujumla.

Pia tamasha hilo litaangalia changamoto zilizojitokeza ndani ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa TGNP mwaka 1993 hapa nchini na kuangalia namna ambayo zitatatuliwa.

"Dhima ya tamasha hilo ni miaka 30 ya TGNP na TAPO la ukombozi wa mwanamke.

Dhima hiyo inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa TGNP.

Katika tamasha hilo pia kutakuwa na mada mbalimbali zitakazo tolewa, watu watatoa uzoefu wao walivyofanikiwa ikiwa pamoja na kukutanisha watu mbalimbali wa vituo vya maarifa na taarifa kutoka kila mkoa.

Akizungumzia kuhusiana na namna ya kushiriki tamasha hilo, Monica amesema kuwa dirisha la kujisajiri litafunguliwa hivi karibuni ingawa tayari mialiko imeshatolewa kwa baadhi ya watu mbalimbali kutengemea na wanakotoka.

Monica ameeleza kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti kwani watakuwa wanasheherekea miaka 30 ya TGNP na kuadhimisha TAPO la Ukombozi wa mwanamke Tanzania, pia katika tamasha hilo wataangalia marekebisho ya sera na sheria zilizofanyiwa marekebisho tangu kuanzishwa wa TGNP hapa nchini.

Pia tamasha hilo litaangazia changamoto ambazo bado zinakwamisha Tanzania kutokuwa na usawa wa kijinsia na namna ya kutatua changamoto hizo.

Kwa upande wa Mwanaharakati Abas Ndelu, amesema kuwa kupitia TGNP ameweza kuhudhuria matamasha matano. Kwa mwaka huu amesema litakuwa tofauti kwani ni muunganiko wa maadhimisho ya miaka 30 ya mtandao huo tangu.

Amesema kuwa amepata manufaa makubwa ya kujitambua, kujua haki mbalimbali za binadamu, haki za wanawake pamoja na kujua sheria mbalimbali hivyo miaka 30 ya TGNP inamafanikio mengi kwao wenyewe pamoja na makundi mbalimbali.

Akizungumzia na mafanikio ya TGNP tangu kuanzishwa kwake, Taraka Seif, maarufu eneo la mabibo Taraka Nyange amesema kuwa Mtandao huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani yeye amepata elimu kutoka katika mtandao huo huku akijizolea umaarufu katika mitaa mbalimbali ya mabibo kwa kutetea haki za wanawake na watoto.

"Imefika mahali inapotokea mama au baba au mtu yeyote anamfanyia ukatili mtoto au mwanamke jamii inasema "Tutaenda kumwambia mama Taraka Nyange" hilo linanipa ujasiri sana wa kuendelea kupambana na ukatili katika mtaa wangu." Amesema Taraka

Kwa upande wa mwanaharakati aliyejiunga na TGNP tangu 2014, Mama Kunambi amesema kuwa TGNP imemtoa uoga kwani mwanzo alikuwa hathubutu hata kumkemea ndugu yake akifanya ukatili, lakini kwa sasa anaweza kwenda mahali popote kwenda kuripoti ukatili unapotokea.

Amesema kuwa mtaani kwake jamii inaogopa kufanya ukatili kutokana na yeye kuwepo katika mahali hapo. Amesema kwa upande wake Mafanikio Makubwa ya TGNP kwa miaka 30 ni kuwatoa woga wananchi ili waweze kugombea nafasi za uongozi na kushauri kuhusiana na bajeti yenye mrengo wa kijinsia kuanzia ngazi ya kifamilia kutokana na kila mwanafamilia kuwa na mahitaji yake.

"Kuelekea miaka 30 ijayo TGNP naomba izidi kupaza sauti ifike mpaka vijijini ili kila mmoja apate uelewa wa mambo ya kijinsia ili kusiwepo mtu ambaye atakatiliwa hata kwa bahati mbaya." Ameeleza.


Afisa Mawasiliano wa TGNP, Monica John akifungua Semina ya Waandishi wa habari kuelekea tamasha la 15 la kijinsia nchini ambalo litaanza Novemba 7-10, 2023 katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam. Semina hiyo imefanyika leo Septemba 2,2023. Jijini Dar es Salaam

Mwasilishaji Bi. Rose Mwalongo akizugumza katika Semina ya Waandishi wa habari kuelekea tamasha la 15 la kijinsia nchini ambalo litaanza Novemba 7-10, 2023 katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.Semina hiyo imefanyika leo Septemba 2,2023.
Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba akizugumza katika Semina ya Waandishi wa habari kuelekea tamasha la 15 la kijinsia nchini ambalo litaanza Novemba 7-10, 2023 katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.Semina hiyo imefanyika leo Septemba 2,2023.
Mhariri wa gazeti la Nipashe Bi.Salome Kitomary akizugumza katika Semina ya Waandishi wa habari kuelekea tamasha la 15 la kijinsia nchini ambalo litaanza Novemba 7-10, 2023 katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.Semina hiyo imefanyika leo Septemba 2,2023.

Mwandishi wa Channel Ten Bi.Dorcas Raymos akizugumza katika Semina ya Waandishi wa habari kuelekea tamasha la 15 la kijinsia nchini ambalo litaanza Novemba 7-10, 2023 katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.Semina hiyo imefanyika leo Septemba 2,2023.
Mwandishi wa EATV Bw.David Gumbo akizugumza katika Semina ya Waandishi wa habari kuelekea tamasha la 15 la kijinsia nchini ambalo litaanza Novemba 7-10, 2023 katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.Semina hiyo imefanyika leo Septemba 2,2023.


Post a Comment

0 Comments