Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. MWINYI AFUNGUA MKUTANO WA KUMI WA AFYA TANZANIA JIJINI DAR ES SALAAM.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati akiufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu leo 3-10-2023.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua mkutano huo, unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 3-10-2023 na (kushoto kwake) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr. John Jungu.(Picha na Ikulu)

WASHIRIKI wa Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akihutubia na kuufungua mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu leo 3-10-2023, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Afisa Masoko wa Hospitali ya Aga Khan Tanzania Rukhsar Kanji , wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Taasisi mbalimbali za Afya Tanzania, kabla ya kuufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) uliofanyika leo 3-10-2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu na Viongozi wengine wa Wizara ya Afya alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania.(Tanzania Health Summit) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hasan, uliofanyika leo 3-10-2023.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments