Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO, BALOZI WA NORWAY WATETA USHIRIKIANO WA NISHATI SAFI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tine Tonnes.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam Novemba 21, 2023 viongozi hao wamejadili kuhusu utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia.

Dkt. Jafo amemueleza Balozi Tinnes dhamira ya Serikali katika kuimarisha upatikanaji wa nishati safi na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kwa kuanza na taasisi zenye kulisha idadi kubwa ya watu.

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha mradi wa nishati ya gesi kusini mwa Tanzania ambao utakuwa chachu katika hifadhi ya mazingira.

Aidha, Waziri Jafo ameishukuru Serikali ya Norway kwa kuiunga mkono Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zikiwemo utoaji wa fedha zaidi ya shilingi 16 hivi karibuni.

"Tunaishukuru sana Norway kwa kuwa nasi bega kwa bega katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na tunaweza kukumbuka tulisaini makubaliano ambayo yalitupatia zaidi ya shilingi bilioni 7 na ule mradi wa utafiti COSTECH bilioni 9 hayo yote ni matunda ya uhusiano baina yetu," amesema Dkt. Jafo.

Kwa upande wake Balozi Tinnes amesema kuwa dhamira ya Serikali yake ni kuwekeza katika miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ameelezea dhamira ya kampuni mbalimbali kutoka Norway kuwekeza katika gesi ambayo itasaidi kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya nishati ya kupikia.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tine Tonnes katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam Novemba 21, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tine Tonnes mara baada ya mazungumzo yao katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tine Tonnes mara baada ya mazungumzo yao katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam. Wengine kuanzia kulia ni Mshauri wa Nishati kutoka ubalozini Bw. Isdory Fitwangile, Mhandisi Mwanaasha Tumbo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Mshauri wa Kilimo kutoka ubalozini Bw. Kassim Mkwizu.

Post a Comment

0 Comments