Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB YAKABIDHI MAGODORO KWA SHULE YA SEKONDARI ZIBA BAADA YA BWENI KUTEKETEA KWA MOTO

Benki ya CRDB imekabidhi Magodoro na madaftari kwa Shule ya Sekondari Ziba iliyopo wilaya ya Igunga Mkoani Tabora  kufuatia bweni la Wavulana kuteketea kwa moto Januari 23,2024 na kuteketeza vyote vilivyokuwa ndani ya bweni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo Jumatano Januari 24, 2024, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wambura Wagana amesema Benki ya CRDB inatoa pole kwa shule hiyo kufuatia tukio hilo hivyo imekabidhi magodoro na madaftari ili kusaidia kutatua changamoto zilizojitokeza.

"Ndugu zangu Viongozi mkiongozwa na Mhe. Mkuu wa wilaya, walimu, Wazazi, wanafunzi ninyi mmekuwa wadau wa Benki ya CRDB wakubwa hivyo lazima tuungane kwenye shida na raha. Tulipopata taarifa ya janga hili tuliona tuje kuwapa pole na kuwakabidhi magodoro na madaftari kwani tumeambiwa mmeunguliwa vitu vyote bwenini", amesema Wagana.

 Akipokea msaada huo kutoka Benki ya CRDB, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa wilaya ya Igunga Mhe. Sauda Mtondoo ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo wa magodoro na madaftari na kuwaomba wadau wengine waendelee kuwashika mkono.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wambura Wagana (kushoto) akikabidhi magodoro na vifaa vya shule kwa Mkuu wa wilaya ya Igunga Mhe. Sauda Mtondoo kufuatia bweni la shule ya Sekondari Ziba kuteketea kwa motoPost a Comment

0 Comments