Ticker

6/recent/ticker-posts

KINANA ASHAURI WANANCHI WAPEWE NAFASI KUAMUA MASUALA YA MAENDELEO YAO

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdulrahman Kinana ameshauri kuwa umefika wakati mambo ya msingi yanayohusu maendeleo ya wananchi lazima yaamriwe na yatokane na wananchi wenyewe.

Amesema japokuwa wapo wawakilishi wa wananchi wakiwemo wabunge, madiwani au halmashauri, lakini hawana uwezo wa kubadilisha hali iliyopo, hivyo ni muhimu wananchi wakapata nguvu zaidi kushiriki kuamua mambo ya muhimu kwao.

Kinana ametoa ushauri huo alipozungumza na wanachama wa CCM na wanachi wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi baada ya kuzindua Shina la Chama, Majengo Sokoni.

Akielezea zaidi kuhusu umuhimu wa wananchi kushirikishwa katika kuamua maendeleo alitoa mfano kuna wakati akiwa Katibu Mkuu wa CCM akiwa na Nape Nnauye walienda wilayani Ngorongoro wakafanya mkutano mkubwa.

"Tulipokuwa pale ukitazama pale kwa mimi ungeniuliza ningesema wale wananchi wanahitaji maji lakini tulipouliza wenyeji wakasema tatizo lao si maji bali ni mtandao wa simu.

"Unaweza ukaona wewe unakwenda mahali ukifikiri shida ya watu ni shule, ni maji kumbe shida yao ni jambo jingine kabisa ndio ni lazima tuwashirikishe wananchi.

"Katika kuamua mambo yanayohusu maisha yao, tusichukue amana ya kuwafikiria , tusichukue mamlaka ya kuwaamria.Ni vizuri tukae na wananchi tuzungumze nao ili watuambie kitu gani wanakihitaji kwa wakati gani na kwasababu gani, ", amesema Kinana

Amefafanua kuwa ukiwaambia wananchi leo wajitolee kujenga barabara wanaweza kukwambia wao wanataka shule kwanza huku akieleza katika mkutano huo imezungumzwa kuhusu kupeleka madaraka kwa wananchi.

"Kwahiyo uundwaji wa vijiji, vitongoji, ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi. Ukiangalia nchi yetu ilivyokaa wakati wa Uhuru katika miaka ya 1960 na 1970 tulikuwa na mikoa tisa leo tunamikoa zaidi ya 30.Tulikuwa na wilaya 50 leo tunakaribia wilaya 200 , tulikuwa na kata chache leo tunakata nyingi

"Kwa hiyo Mwenyekiti na Mbunge nimewasikia kuhusu madaraka kwa wananchi.Tupeleke uamuzi kwa wananchi uhwe na tija lazima kuwe na taasisi inayosaidia wananchi kufanya maamuzi hayo.

" Kwa hiyo nawashukuru umetoa wazo hilo na nitalichukua kwenda kushauriana na wenzangu.Nitatoa maoni na ushauri.Nadhani kuna jambo linabidi vile vile tulijadili , tunapenda sana kukabidhi maamuzi ya muundo wa nchi yetu kwenye kikundi kidogo cha watalaamu.

"Ndio maana wakati mwingine unaweza ukawa na mantinki na ukawa na hoja ya kuwa na kijiji au kuwa na mtaa au kuwa na serikali fulani mahala fulani lakini kwasababu wanaoamua wako mbinguni, wako kule juu lazima maombi yapelekwe mbinguni kwa wakubwa."

Alisisitiza kuwa hiyo inamfanya afikiri mambo ya msingi yanayohusu maendeleo ya wananchi lazima yaamriwe na wananchi na lazima yatokane na wananchi.Wabunge wanaona jambo jema , halmashauri kuu ya wilaya inaona jambo jema , madiwani wanaona jambo nzuri, lakini hawana uamuzi nalo."

Hivyo amesema umefika wakati kama kweli madaraka ni ya wananchi, basi wawakilishi wa wananchi wawakilishe wananchi, wawe na kauli katika kuamua juu ya mambo yanayohusu wananchi tusibaki na mfumo na utaratibu wa zamani.

UTEKELEZAJI ILANI MTAMA

Aidha, alipongeza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM unaofanywa katika Jimbo la Mtama, alisema kazi nzuri inafanyika kupitia kwa madiwani na viongozi wa halmashauri katika kusimamia utekelezaji wake.

"Nampongeza Mbunge wenu Nape anatosha. Ni kijana hodari anajituma, nimekaa naye miaka saba, spidi yake ilikuwa kali, kuna wakati nilikuwa naipunguza na nilimwambia Nape jifunze kuwa na subira na siku hizi anasubira kuliko mimi."

Kinana alisema kuwa amesomewa taarifa ya Chama na taarifa ya Serikali, nikaangalia kila eneo, umeme vijijini kwa mfano Mkoa wa Lindi kabla ya kufikia Desemba 2025 vijiji vyote vitakuwa na umeme.

"Mimi nina bahati ya kuzunguka nchini, hivi karibuni nilikuwa Geita na Kagera , na kabla ya hapo nilikuwa Manyara, Tabora na sehemu nyingine.Nataka niwahakikishie ndugu zangu itakapofika 2025 vijiji vyote nchi hii vitakuwa na umeme."

Pia, amesema wakati mwingine amekuwa akisikia watu wanamalalamiko ya maji , umeme , afya na mengine lakini akisikia malalamiko hayamtishi bali yanamtia ari.

"Malalamiko ni matokeo ya kazi nzuri inayofanyika , kila tukipiga hatua watu wanadai hatua mara mbili, sio wanalalamika kazi haifanyiki hapana, wanasema kama mmeweza kufanya kiasi hiki tunaomba basi mfanye mara mbili, mara tatu, mara nne.

"Maana yake kama mmeweza kupeleka umeme vijiji vyote sasa tunataka mpeleke kwenye vitongoji na mitaa yote , ndio maana yake, maendeleo yanaleta hamu kubwa zaidi ya maendeleo.Kwa hiyo yanaleta madai makubwa zaidi, ", amesema Kinana.

Aliongeza kwamba katika mkutano huo wananchi wamemsikia Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afyav look mm(NHIF) Mkoa wa Lindi, Irene Kataraihya akizungumza kuhusu bima ya afya, kuna sheria imepitishwa bungeni.

"Jambo moja hajawaaambia sheria hii imerudi bungeni mara nne, mara ya kwanza ikaboreshwa, mara ya pili ikaboreshwa, mara ya tatu ikaboreshwa na mara ya nne hatimaye ikapita kuwa sheria.

"Lengo ake ni moja kumpa huduma bora kila Mtanzania na hata hizi kelele ndogondogo mnazosikia ni kelele la kufanya jambo lenyewe liwe nzuri zaidi.Kwa hiyo nikisikia kelele watu wanazungumza changamoto unakaa unatakari unasema hapa watu wanachotaka jambo hilo liwe nzuri zaidi.

ALICHOSEMA NAPE

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alikiomba Chama kutazama upya uamuzi wa kutanua maeneo ya kiutawala hususan kwa ngazi ya vijiji na vitongoni.

Kwa mujibu wa Nape, baadhi ya maeneo kuna hali ngumu kuwahudumia wananchi kutokana na ukubwa wa maeneo na wingi wa wananchi hivyo ni vyema kuridhia kuyaongezea maeneo ya kiutawala.

Nape alisema kuwa kutokana na wingi huo na umuhimu wa kuwahudumia wananchi, alikiomba Chama kiridhie kuanzishwa kwa vijiji na vitongoni vipya kusaidia kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, alisema serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk, Samia Suluhu Hassan amefikisha huduma mbalimbali za muhimu katika Jimbo hilo.

Miongoni mwa huduma hizo ni maji safi na salama, ujenzi wa vituko vya afya na zahanati, kufungua mawasiliano ya simu za mkononi na kusambazia umeme.

Kwa upande wake Meneja wa NHF Lindi, Irene alikiomba Chama kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na huduma hizo kujihakikishia matibabu wakati wote.

Ali Likalqmbile mkazi wa Kijiji cha Londo wilayani humo, alimpongeza Kinana kwa kuona umuhimu wa wananchi kushirishwa katika kuamua mambo yanayohusu maendeleo yao.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akizungumza baada ya kuzindua Shina la Wakereketwa wa CCM Majengo Sokoni.(Picha na Fahadi Siraji)

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoan I alındı ambale pia ni Waziri was Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa Barbara uliofanyika Majengo Sokoni Jimbo humo baya ya uzinduzi wa Shina la CCM Majengo Sokoni uliofanywa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, leo.

Makamu Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wanachama wa Shina Namba Moja Majengo Sokoni alipowasili kufungua shina hilo katika Jimbo la Mtama.

Post a Comment

0 Comments