Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. NCHIMBI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MABALOZI WA NCHI SITA MARAFIKI ZA KUSINI MWA AFRIKA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, pamoja na baadhi ya Mabalozi wa Nchi Sita Marafiki za Kusini mwa Afrika, wakiwa wamesimama kimya kwa dakika moja, kuomboleza na kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Namibia, Hayati Komredi Hage Gottfried Geingob, kabla ya kuanza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali, yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar Es Salaam. Kulia kwa Dkt. Nchimbi ni Balozi wa Angola, Mhe. Sandro de Oliveira, akifuatiwa na Balozi wa Msumbiji, Mhe. Ricardo Mtumbuida na anayefuata ni Balozi wa Afrika ya Kusini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe. Nchi zinazounda urafiki huo wa kihistoria na Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika, vinavyoongoza nchi hizo ni Tanzania (CCM), Angola (MPLA), Msumbiji (FRELIMO), Zimbabwe (ZANU – PF), Namibia (SWAPO) na Afrika Kusini (ANC).

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na mabalozi wa nchi za Angola, Msumbiji na Afrika Kusini, wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania, ambazo ni sehemu ya Nchi Sita Marafiki za Kusini mwa Afrika (zingine ni Tanzania, Zimbabwe na Namibia), alipokutana nao Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, Jumatatu, Februari 5, 2024, kujadiliana masuala mbalimbali. Mabalozi hao walioko pichani ni Mhe. Sandro de Oliveira (Angola), Mhe. Ricardo Mtumbuida (Msumbiji) na Mhe. Noluthando Mayende-Malepe (Afrika Kusini).

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Angola, Mhe. Sandro de Oliveira (kushoto pichani), Balozi wa Msumbiji, Mhe. Balozi Ricardo Mtumbuida (kulia pichani) na Balozi wa Afrika ya Kusini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe (kushoto kwa Dkt. Nchimbi), baada ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali, leo Jumatatu, Februari 5, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam,

Post a Comment

0 Comments