Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS MSTAAFU NA MWENYEKITI WA GPE DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA VIKAO VYA BODI HIYO MJINI BERLIN, UJERUMANI

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education - GPE) akiongoza Vikao vya Bodi ya Taasisi hiyo vinavyofanyika Jijini Berlin, nchini Ujerumani kuanzia tarehe 4 - 6 Juni, 2024.

Katika vikao hivyo, Taasisi ya GPE inapitia na kuazimia masuala mbalimbali ya kiundeshaji yatakayolenga kuboresha mifumo ya elimu katika nchi zinazoendelea ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu na kuhakikisha wanapata elimu iliyokusudiwa.
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education) - GPE) akiwa na Mhe. Svenja Schulze, Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani aliyeshiriki katika ufunguzi wa vikao hivyo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa GPE Bi. Laura Fringeti
Vikao vya Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education - GPE) vikiendelea chini ya : Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi hiyo vinavyofanyika Jijini Berlin, nchini Ujerumani kuanzia tarehe 4 - 6 Juni, 2024.
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education - GPE) a kibadilishana mawazo na wajumbe wakati wa mapumziko ya Vikao vya Bodi ya Taasisi hiyo vinavyofanyika Jijini Berlin, nchini Ujerumani kuanzia tarehe 4 - 6 Juni, 2024.

Post a Comment

0 Comments