Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIGO LA EURO CUP NA HISENSE HALIPOI , WENGINE TENA WAJISHINDIA TIKETI , FRIJI NA TV ZA HISENSE

  

Emmanuel Mlonjela - Mhandisi Mkazi wa Dar es Salaam ( Kushoto ) ambaye ni mshindi wa tiketi ( Wiki ya Pili ) Kampeni ya ZIGO la EURO CUP na Hisense, safari iliyolipiwa kila kitu  kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora, akikabidhiwa Mfano wa Tiketi tukio lililofanyika mapema leo hii June , 07 , 2024 Makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es Salaam , Mhandisi Emmanuel ameibuka mshindi baada ya kubashiri Mechi na PariMatch kupitia Tigo Pesa Super App, Kulia ni Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta na katikati ni Erick Gerald kutoka PariMatch.

Na Adery Masta.

Mhandisi Emmanuel Mlonjela Mkazi wa Dar Es Salaam, ni Mteja wa Tigo wa pili kujishindia Safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda kutazama Mechi za Kombe la EURO 2024 , ambapo timu 24 zinatarajiwa kuchuana katika miji 10 mwenyeji Nchini Ujerumani . 

Emmanuel ameshinda kupitia Kampeni ya ZIGO LA EURO CUP NA Hisense , iliyozinduliwa wiki kadhaa Zilizopita ambapo Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO, kwa kushirikiana na Parimatch na Hisense waliileta kusambaza Tabasamu kwa Wateja wao.

Ili kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia tiketi au zawadi ya fedha taslimu TZS 1,000,000, na Vifaa vya Hisense TV na Friji washiriki wanapaswa kujiandikisha na Parimatch, kuweka pesa zao kupitia Tigo Pesa kisha kuweka dau ( betting ) kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu na Parimatch. Kadiri dau zinavyowekwa, ndivyo nafasi zinavyoongezeka ya kushinda TZS 1,000,000 au tiketi ya safari na mechi yenye malipo kamili ya kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora.


Akizungumza Wakati wa Kugawa zawadi kwa Washindi ambao kati Yao ni Washindi wawili wa Kifurushi cha Vifaa vya Kielekitroniki kutoka Hisense ambavyo ni TV janja na Friji la kisasa , Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema 

" Ndo kwanza ni droo ya pili ya Kampeni yetu ya ZIGO LA EURO na Hisense , kama ambavyo inajulikana Kampeni hii tunatafuta Washindi wa Tiketi ya Kwenda kushuhudia Mechi za Euro , Washindi wa Vifaa vya Hisense ambavyo ni Friji na Tv ya Kisasa , na Washindi wa Pesa Taslimu

Mmoja kati ya Washindi wa Vifaa vya Hisense ambavyo ni Friji na Tv ( kushoto ) katika picha na mwakilishi kutoka Hisense Bw. Ally Hamis ( kulia )

Zawadi bado zipo nyingi kwa maana Leo ndo Washindi wa Droo ya pili, bado Kuna Droo nyingine sita zinawasubiri , Tumia kwa wingi TIGO Pesa Super App , Bashiri na Parimatch kupia App ya Tigo Pesa ili kutengeneza mazingira ya kujishindia zawadi za Tv na Friji kutoka Hisense , Fedha Taslimu Hadi Milioni Moja na Zawadi kubwa ya kwenda kushuhudia Mechi za EURO CUP 2024 " alimalizia Mary Ruta


Post a Comment

0 Comments