Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa hadhara Mjini Shinyanga, akitoa shukrani kwa imani waliyoionesha katika Uchaguzi Mkuu kwa kumchagua kuwa Mbunge, kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuwachagua madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Na Paschazia Charles - Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, ameahidi kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo kwa kusimamia kwa karibu miradi ya maendeleo katika sekta za miundombinu, maji, afya, elimu na ajira kwa vijana.
Mhe. Katambi amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, na kwamba dhamira hiyo itaendelezwa kwa kasi zaidi katika Jimbo la Shinyanga.
Ameyasema hayo leo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga, uliohudhuriwa na wananchi kutoka Jimbo la Shinyanga na maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Katambi amesema ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, mafanikio makubwa yamepatikana ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kimkakati kama madaraja, reli ya kisasa (SGR), barabara, shule na hospitali, sambamba na juhudi za kuinua uchumi wa wananchi hususan vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Shinyanga kwa kuendelea kuiamini CCM na Serikali yake, akisisitiza kuwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi Mkuu ni ushindi wa wananchi wote wenye kiu ya maendeleo, ustawi na amani ya taifa.
Amewashukuru kwa imani waliyoionesha kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga, kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuwachagua madiwani wa CCM, hatua aliyoeleza kuwa inaonesha mshikamano mkubwa na imani ya wananchi kwa uongozi wa chama hicho.
Katika kusisitiza suala la amani, Mhe. Katambi amesema kuwa amani, umoja na utulivu wa nchi ni nguzo muhimu ya maendeleo, akiwahimiza wananchi kuendelea kuilinda na kuitunza. Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao ili kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na kukuza uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mwanahamis Munkunda, amesema Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari imeanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo, akieleza kuwa ndani ya siku mia za mwanzo ajira katika sekta za elimu na afya zimetolewa, utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote umeanza pamoja na hatua za uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kuendelea kutekelezwa.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.

0 Comments