Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE MAKUBEL AANZA NA ELIMU AGAWA MADAFTARI SHULE ZA MSINGI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI




Na Oscar Assenga, TANGA

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Kassim Amar Makubel ameanza kugawa madaftari kwa wanafunzi wa shule za Msingi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua sekta ya elimu hapa nchini.

Makubel aliyasema hayo wakati wa halfa ya kuzindua zoezi la kugawa Madaftari kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Pongwe kupitia Mpango wa Daftari la Mama Samia kwa kushirikiana na Taasisi ya Watoto Foundation ambapo mpango huo utazifikia shule zote kwenye Jimbo hilo.

Mbunge huyo alisema kwamba mpango huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali na Rais Dkt Samia Suluhu katika sekta ya elimu kutokana na mabadiliko na mageuzi makubwa yaliyofanyika.

Alisema kwamba wakati alipoingia madarakani alikaa na kubaini vijana wengi wa shule ya msingi wanapitia changamoto nyingi hivyo akaona ni bora kila kila mzazi wa mtoto wa Jimbo hilo anayesoma shule ya msingi walau aguse maisha yake kwa kutoa madaftari matano 5 ili kuwapunguzia makali kwenye baadhi ya mahitaji.


Alieleza madaftari hayo ni sehemu ya mchango wake kurejesha shukrani kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu uliopita na wameanza rasmi uzinduzi ambapo wataanza kugawa madaftari hayo Tarafa ya Pongwe na kasha kuelekea kwenye kata nyengine.

Aidha alisema kwamba Tarafa hiyo inayojumuisha Kata za Marungu,Kirare na Pongwe na baadae wataenda kwenye Tarafa nyengine ili kuhakikisha shule zote za misngi zinafikiwa na kuwagusa.



Alisema keamba mabadiliko hayo yaliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu katika sekta ya elimu wakati alipoingia madarakani ni kuona elimu walionayo haikizi mahitaji ya sasa na wanatakiwa kuendana na mabadiliko kwenye mitaa ya elimu ya sasa na sasa watoto watasoma darasa la kwanza mpaka la sita.



Aidha alisema mabadiliko hayo machache ikiwemo mkondo wa amali ambao ni muhimu kwa ajili ya kuwapatia ujuzi watoto wanapomaliza shule jambo ambalo litasaidia kuongeza wataalamu mbalimbali ambao watakuwa na mchango mkubwa wa kuweza kujiajiri na kuweza kujiendeleza kwenye vyuo vya kati

“Kutokana na mabadiliko hayo makubwa ya kielimu hapa nchi na hakuna malipo hivyo tuwahimize watoto waende shule pamoja na kufuatilia maendeleo yao na tuhudhurie vikao”Alisema .



Awali akizungumza Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Pongwe Mchanganyiko Abubakari Sadik alimshukuru Mbunge huyo kwa kuwapelekea msaada huo madaftari ambayo yamekuja kutatua changamoto ya watoto ambao hawana uwezo wa kununua madaftari kwa wakati .

"Ukosefu wa daftari ni kwamba wanafunzi asipokuwa na madaftari anakosa kumbukumbu ya kusoma kipindi anapofikia kwenye mtihani yake hivyo msaada huu umeenda kutatua changamoto ya kila mmoja kutokana na wazazi wa watoto wengine wako mbali na inakuwa vigumu kuwa na madaftari kila wakati”Alisema

Alisema kwamba shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika taaluma na wamekuwa na mwendelezo mzuri wa wanafunzi katika madarasa ya mitihani ya darasa la nne.

Aliongeza kwamba changamoto ambazo zinawakabili ni upungufu wa madarasa unaotokana na ongezeo la uandikishaji wanafunzi kila mwaka na wale wanaohamia kutoka maeneo mengine huku akieleza jambo linguine ni bima za afya kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

“Tunamshukuru Mhe Mbunge Wetu kwa kutupelekea wadau wenye kuwasaidia madaftar mchango huo umewapa faraja kubwa na matumaini motisha mpya kwa watoto wao kuonyesha dhamira ya kweli kujenga jamii inayojali na kuthamini kila mtoto bila ubaguzi”Alisema

Hata hiyo alitoa shukrani zake kwa Rais Dkt Samia Suluhu katika kukuza na kutoa kipaumbeme kwenye elimu jumuishi na kupitia uongozi wake fursa za elimu zinaendelelea kuimarishwa na kuwafikia hata wenye mahitaji maalumu.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Watoto Foundation Ally Yakub Pingizi alisema taasisi hiyo imezindua mpango unaoitwa Daftari la Mama Soma na Samia ikiwa ni kipaumbele kuhakikisha wanafunzi hawana sababu ya kutoroka shule ikiwa hana vitendea kazi cha shule.

Alisema kwamba wao wamekuja na mpango wa daftari la mama soma na samia ikiwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu katika kuboresha sekta ta elimu na amefanya maboresho makubwa kwa kujenga miundombinu ya elimu, nyumba za walimu,mabweni na vyoo.


Alisema kwamba taasisi hiyo kupitia mpango huo wameona wao waunge mkono kwa kutoa vifaa hivyo vitendea kazi na kuwatia moyo watoto wa kike waweze kusoma kwa hari na moyo ili kuepuka kujiingiza kwenye vishawishi na watoto wa kike na hivyo kusoma kwa bidii pamoja na kupunguza utoro shuleni hatua itakayochochea ufaulu.









Post a Comment

0 Comments