Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo ameshiriki Mkutano wa 6 wa Kimataifa wa Kutokomeza Utumikishwaji wa Mtoto (6th Global Conference on the Elimination of Child Labour) uliofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 13 Februari, 2026 Marrakech, Morocco.
Aidha, Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) ambalo limewaleta pamoja Mawaziri na wadau kutoka nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kujadili na kukubaliana mikakati madhubuti ya kutokomeza utumikishwaji wa watoto ifikapo mwaka 2030.
Akiwa katika Mkutano huo, Naibu Waziri Kisuo alipata fursa ya kuwasilisha mafanikio ya Tanzania katika kukabiliana na Utumikishwaji wa Mtoto ambapo kiwango cha kimepungua kwa asilimia 9.1 kutoka asilimia 33.8 mwaka 2014 hadi asilimia 25.8 mwaka 2024, kwa mujibu wa Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2024.
Vilevile, Mhe. Kisuo alisema Serikali inaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha watoto wote wanalindwa, wanapata elimu bora na fursa sawa za maendeleo.


0 Comments