NA EMMANUEL MBATILO, TANGA
CHUO Kikuu Mzumbe kimebahatika kuwa kati ya vyuo vikuu 14 na vyuo vya kati 5 vinavyofaidika na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) Chuo kikuu Mzumbe Kimetengewa kiasi cha Dola za Kimarekani millioni 21 (TZS 48,046,740,000.00 ) kwa ajili ya uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia katika Kampasi Kuu na kuanzisha Kampasi mpya katika Mkoa wa Tanga.
Jumla ya miradi ya ujenzi wa miundombinu saba (7) inajengwa katika Kampasi ya Tanga ambapo miradi hiyo imegawanywa katika Lot mbili ili kuongeza ufanisi. Lot zote mbili zinajengwa na Mkandarasi DIMETOCLASA Realhope Limited kwa kushirikiana na MPONELA Construction Company Limited chini ya usimamizi wa Kampuni ya Mekon Arch. Consult Limited. Lot zote zinajengwa na mkandarasi DIMETOCLASA Realhope Limited.

Chuo hicho kinajengwa katika kata ya Gombero, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga,
Maelezo ya Mradi
Mikataba ya ujenzi wa Lot zote mbili ilisainiwa tarehe 30.8.2024 na kazi ya ujenzi ilianza rasmi. Kazi za ujenzi zilitarajiwa kukamilika tarehe 30 Novemba 2025. Hata hivyo kazi hazikukamilika na mkandarasi aliomba kuongezewa muda wa ziada, ambapo sasa kazi hizo zinatarajiwa kukamilika tarehe 28 Februari 2026.
Miradi inayoendelea kutekelezwa kupitia mpango huo ni Ujenzi wa Jengo la Taaluma lenye jumla ya madarasa 6, Maktaba ndogo, Ukumbi wa mihadhara, maabara mbili zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila moja, pamoja na ofisi 36 zitakazohudumia wafanyakazi 72.
Aidha majengo mengine ni Hosteli 2 za wanafunzi, Bwalo la Chakula, Kituo cha afya kitakachohudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa vijiji vilivyopo jirani na Chuo, Nyumba 4 za Wafanyakazi, Mfumo ya majitaka na dampo la kuhifadhia taka ngumu pamoja na Tenki la kuhifadhi Maji Safi la ujazo wa lita laki 4.
Maendeleo ya Ujenzi (Kampasi ya Tanga – Lot 1)
i) Ujenzi wa jengo la taaluma (Academic Building) Ujenzi unaendelea na umefikia asilimia 77.
ii) Ujenzi wa Kituo cha Afya (Health Centre Buidling)
iii) Ujenzi wa jengo la kafeteria (Cafeteria Building) Ujenzi unaendelea na umefikia asilimia 82.
Maendeleo ya Ujenzi (Lot 2)
ii) Ujenzi wa mabweni ya wanafunzi (student hostel) Ujenzi unaendelea na umefikia asilimia 74.
iii) Ujenzi wa miundombinu ya maji safi na tanki la kuhifadhia Maji Ujenzi wa Miundombinu na tank la maji safi umefikia asilimia 75.
Mkandarasi amemaliza ujenzi wa tanki na anaendelea na kazi za umaliziaji. Shughuli zinazoendelea ni pamoja na upakaji wa plasta ya nje kwenye tanki.Kazi zilizobaki ni kuweka miundombinu ya kutoa maji kwenye visima kupeleka kwenye tanki.
iv) Ujenzi wa mabwawa ya maji taka (Oxidation Ponds)
Ujenzi wa miundombinu ya taka unaendelea na umefikia asilimia 65 ambapo mkandarasi ameshachimba mitaro ya kupitisha mabomba ya maji taka na mabwana na anaendelea na ufungaji wa mabomba ya DPM, kumwaga zege na kuweka nguzo za uzio. Pia ameanza kuchimba msingi wa ujenzi wa vizimba vya taka ngumu.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi Februari 15, 2026, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alisema: "Mradi huu unaleta heshima na kutoa uhuru wa nchi. Umetekelezwa kwa ubora na thamani ya fedha inaonekana."



























0 Comments