Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akizungumza na ujumbe wa Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026.
***************
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Machi 06, 2026 Jijini Dar es Salaam, ujumbe huo ulifanya ziara kwa ajili ya kujitambulisha na kuwasilisha maombi ya ushirikiano baina yake na Serikali.
Kupitia mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo hicho Prof. Gabriel Miguel alieleza masuala mbalimbali ikiwemo muundo na shughuli za kituo na miradi iliyotekelezwa katika nchi wanachama.
Kwa mujibu wa Prof. Miguel ameeleza utaratibu wa kujiunga na mtandao wa kituo hicho kwa nchi wanachama unaobainisha fursa na faida mbalimbali ikiwemo mapambano ya mabadiliko ya tabianchi, usimamizi endelevu wa ardhi na uhifadhi wa mazingira.
Aidha ameeleza kuwa taasisi hiyo imeendelea kujenga uwezo wa kitaalamu katika masuala ya kiufundi, ujenzi wa miundombonu na programu za masomo ya elimu ya juu kwa wataalamu katika nchi wanachama.
“Kituo kimefanya tafiti za masuala ya kilimo hifadhi, bayoanuai, mifumo ikolojia na nishati mbadala na kuhakikisha matokeo ya tafiti hizi yanaakisi mipango ya maendeleo katika nchi wanachama” amesema Prof. Miguel.
Prof. Miguel ameeleza kuwa kituo hicho kimekuwa kikifanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Serikali, mashirika ya mazingira, wadau wa viwanda na taasisi za kikanda.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amekishukuru kituo hicho kwa kufanya ziara Tanzania na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha uhifadhi endelevu wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha Dkt. Muyungi alieleza dhamira dhati ya Serikali kujiunga na kituo hicho ambapo aliainisha vipaumbele na maeneo ya ushirikiano ambayo ni muhimu kuzingatiwa kulingana na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo.
“Tunashukuru kwa ziara hii ambayo imekusudia kuimarisha wigo wa ushirikiano katika nyanja ya sayansi, hili ni jambo muhimu kwa Serikali ya Tanzania hususani katika kipindi hiki tunachoelekea katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa 2050” amesema Dkt. Muyungi.
Dkt. Muyungi pia alitoa ushauri kuhusu umuhimu wa kuundwa kwa timu ya pamoja ya wataalamu kati ya kituo na wataalamu watakaopendezwa na serikali ili kujadili kwa kina kuhusu faida zitakazopatikana iwapo Tanzania itaridhia kujiunga na taasisi hiyo.
SASSCAL ni kituo cha utafiti kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi, tathimini ya mazingira na usimamizi endelevu wa mazingira. Nchi wanachama wa Kituo hicho ni Angola, Botswana, Namibia na Afrika Kusini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akizungumza na ujumbe wa Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Mhe. Balozi Baraka Luvanda
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akizungumza na ujumbe wa Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Mhe. Balozi Baraka Luvanda na Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Dkt. Kaninzio Manyika
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akizungumza na ujumbe wa Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Mhe. Balozi Baraka Luvanda na Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Dkt. Kaninzio Manyika
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL)Prof. Nelaga Indongo (katikati) akizungumza wakati wa kikao baina yao na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026. Kulia ni Kiongozi wa ujumbe huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo hicho, Prof. Gabriel Miguel.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) Prof. Gabriel Miguel akizungumza jambo wakati wa kikao baina yao na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Prof. Nelaga Indongo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Kaninzio Manyika akizungumza jambo wakati wa kikao baina yao na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kushoto) na Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda (katikati) akizungumza jambo wakati wa kikao baina yao na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi na Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026. Kuliani Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akipokea nakala ya taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Kituo cha cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo hicho Prof. Gabriel Miguel muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akipokea nakala ya taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Kituo cha cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Prof. Nelago Indongo muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kituo cha Umahiri wa Masuala ya Sayansi na Usimamizi Endelevu wa Ardhi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SASSCAL)uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo hicho Prof. Gabrel Miguel muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao Jijini Dar es Salaam Machi 06, 2026.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)









0 Comments