Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. SAJAD HABIB RAI; MBUNIFU ‘KITANZI’ CHA WAKWEPA KODI KWA WAFANYABIASHARA WA MAFUTA

 


*Ampongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa uchapakazi

*Asisitiza Tanzania itavuka salama Kipindi hiki kigumu cha tatizo la mafuta 

Na Mwandishi Wetu

"KAMA ambavyo imejaaliwa kuwa na aina mbalimbali ya vivutio vya Utalii,Mali asili,  yakiwemo madini na vinginevyo, pia hivyo Taifa la Tanzania limejaaliwa kuwa na viongozi hodari tangu ilipopata uhuru wake Mwaka 1961"

"Ukiacha viongozi wengine waliotangulia na kuliongoza Taifa hili,kwa sasa tunaye Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye kwa hakika watanzania wengi tunajivunia uongozi wake imara tangu aliposhika madaraka kutuongoza" ameanza kwa kusema hivyo Dkt.Sajad Habib Rai

Dkt.Sajad anayehudumu kama Meneja wa nchi katika Bohari ya kuhifadhia mafuta Jamii ya Petroli 'MOIL Energies' , anasema kupitia utawala wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kila jambo ndani ya nchi linakwenda sawa likiweko suala zima la nafasi kwa wawekezaji kufanya uwekezaji nchini.

"Hakika kwa hili Rais Samia anastahili pongezi, ameifanya Tanzania kuwa kimbilio la watu kutoka Mataifa ya nje kuja na kuwekeza, fursa hiyo haipo katika kila Taifa, hapa ndipo unaona uhodari wa Kiongozi huyu" anasema Dkt.Sajad

Kimsingi mtaalamu huyu katika fani za Ununuzi na Ugavi, usafirishaji, biashara katika Tasnia ya nishati ya mafuta akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 20, kwake ni fahari kutekeleza majukumu yake chini ya utawala wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan 

"Kiongozi bora ni yule anayejulikana kwa kujenga timu zenye mshikamano, kuendesha ufanisi wa utendaji kazi, na kukuza utamaduni wa utendakazi na uwajibikaji, hakika Dkt.Samia amejitolea kufanya kazi kwa ubora, pamoja na mambo mengine hilo ni jambo pekee linalotufanya tufurahie uongozi wake" amesisitiza Dkt Sajad.

Dkt.Sajad kama mmoja wa viongozi wanaotoa mchango mkubwa katika sekta ya mafuta nchini, kupitia nafasi yake ya usimamizi wa bohari ya mafuta, ameonyesha uwezo mkubwa wa kuunganisha maslahi ya wafanyakazi, wawekezaji na Serikali kwa ujumla.

Uongozi wake umeendelea kuonekana kuwa wa vitendo siyo tu kwa timu yake anayoiongoza katika eneo lake la kazi, bali hata maeneo mengine ikiwemo Serikalini, kwani hivi karibuni kupitia mchango wake wa mawazo umesaidia kuleta tija katika eneo la kodi na ushuhuru kipitia biashara ya mafuta.

Kupitia mawazo yake ya kudhibiti vitendo vya ukwepaji kodi kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta akitoa wazo  kuwa kila muagizaji wa mafuta anapaswa kukadiriwa  kodi kulingana na kiasi Cha mafuta alichoagiza kabla ya mafuta hayo kuingia sokoni, kwa kiasi kikubwa kumesaidi kuleta tija.

Anasema wazo hilo ambalo kabla ya kulitoa kulisababisha kuwepo kwa 'ujanja ujanja' kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara kukwepo kodi kumesaidia kuiongezea mwanya Mamlaka ya Mapato ( TRA) kukusanya kodi yake kwa ufasaha hali ambayo pia imesaidia kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Anasema siku zote katika mazingira ya biashara ya mafuta ambayo yanahitaji umakini mkubwa, nidhamu pamoja na uwajibikaji, ameendelea na ataendelea kusimamia utendaji wa kazi kwa weledi mkubwa.

Moja ya mambo yanayomtofautisha ni namna anavyoweka mbele ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi za Serikali, akionesha wazi kuunga mkono mifumo mipya ya usimamizi wa mafuta, ikiwemo ulipaji wa kodi kabla ya mafuta kuingia sokoni. 

Mfumo huu umechangia kupunguza mianya ya ukwepaji kodi sambamba na kuongeza mapato ya Serikali kwa kuleta ushindani wa haki kwa wafanyabiashara wanaofuata sheria.

Mchango wa Dkt Sajad kwa upande wa Serikali  unaonekana katika kuongeza mapato kupitia kodi, kudhibiti upotevu wa mafuta, kuimarisha usalama wa nishati na kusaidia uchumi wa taifa tukielewa pia kuwa Sekta ya mafuta ni mhimili mkubwa wa maendeleo ya nchi, hivyo viongozi wenye maono kama Dkt Sajad wanakuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya taifa.

Aidha akizungumzia changamoto ya mafuta inayoikumba Dunia kwa Sasa, Dkt Sajad anasema hali hiyo siyo kwa Tanzania pekee bali hata upande wa mataifa mengine Duniani ikichangiwa na mzozo unaendelea Mashariki ya Kati ingawa kwa Tanzania bado Kuna akiba ya kutosha ya mafuta.

Dkt Sajad Habib Rai ni mfano wa kiongozi anayejali maendeleo ya wafanyakazi na Taifa kwa pamoja. Utendaji wake umeonyesha kuwa mafanikio siyo kwa taasisi yake tu, bali pia taasisi yoyote inayotegemea uongozi bora, uwajibikaji na uwezo wa kuendana na mabadiliko ya kisasa katika sekta husika, kupitia juhudi zake, sekta ya mafuta inaendelea kuwa na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa Tanzania.



Post a Comment

0 Comments