Ticker

6/recent/ticker-posts

MAREKEBISHO YA SHERIA YA PPP YAFUNGUA FURSA MPYA ZA UWEKEZAJI

Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa sekretarieti za PPPC na TPSF wakati wa mkutano wa ushirikiano wa kimkakati katika warsha ya kujengea uwezo viongozi wa sekta mbalimbali na Wakurugenzi Wakuu kutoka mashirika ya sekta binafsi.

************

Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre), kwa kushirikiana na Jukwaa la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), kimewakutanisha wadau kwa sekta binafsi jijini Dar es Salaam katika mafunzo maalum ya kujenga uwezo kuhusu miradi ya ubia (PPP).

Mafunzo haya yamelenga kutoa uelewa wa kina kuhusu namna Tanzania inavyoweza kutumia kikamilifu mfumo wa PPP kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan katika muktadha wa mabadiliko mapya ya sheria na fursa zilizopo kwenye orodha ya miradi (pipeline).

Kupitia majadiliano ya kitaalamu na uzoefu wa wataalam kutoka sekta binafsi, washiriki wamepata uelewa mpana juu ya nafasi ya sekta binafsi katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku wakihamasishwa kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta za kimkakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila akizungumza wakati wa mkutano wa ushirikiano wa kimkakati katika warsha ya kujengea uwezo viongozi wa sekta mbalimbali na Wakurugenzi Wakuu kutoka mashirika ya sekta binafsi.
Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa sekretarieti za PPPC na TPSF wakati wa mkutano wa ushirikiano wa kimkakati katika warsha ya kujengea uwezo viongozi wa sekta mbalimbali na Wakurugenzi Wakuu kutoka mashirika ya sekta binafsi.

Kikao kililenga kuchambua na kujadili Sheria ya PPP Na. 4 ya mwaka 2023, pamoja na kupitia miradi ya PPP iliyo kwenye mchakato, huku kikirahisisha njia za uwekezaji wa sekta binafsi katika miradi ya mageuzi nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments