Katika kuhakikisha wanafunzi wanamaliza safari yao ya masomo bila vikwazo, hususan vinavyo husiana na afya na ustawi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni - UNESCO kupitia mradi wake wa Haki Zetu, Maisha yetu, Mustakabali Wetu (“Our Rights Our Lives Our Future”) unaofahamika kama O3 kwa kushirikiana na WHO na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya imezindua utafiti wa kimataifa wa afya na sera za afyaskulii.
Tukio hili la uzinduzi pia limejumuisha makabidhiano ya vitabu vya ziada vyahadithi zinazojenga misingi ya afya na ustawi kwa wanafunzi wa skuli za msingi, vinavyolenga kusaidia elimu ya afya na kuendeleza mazingira bora ya skuli.
Utafiti wa “Global School-Based Student Health Survey (GSHS)” na “Global School Health Policies and Practices Survey (G-SHPPS)” ni hatua muhimu katika kuimarisha sera na programu zenye msingi wa ushahidi wa kisayansi zinazokuza afya na ustawi wa watoto na vijana balehe.
Tafiti hizi zinatoa takwimu muhimu kuhusu mienendo ya kiafya, utekelezaji wasera na mipango ya kisecta juu ya uimarishaji wa huduma za afya na ustawi kwa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na maeneo kama vile lishe, afya ya uzazi, afya ya akili, usafi wa mwili, ukuaji wa mwili na ulinzi dhidi ya ukatili . Matokeo ya tafitihizi yatasaidia kuongoza mijadala ya kisera, maboresho ya sera na uandaaji waprogramu za kitaifa zinazowawezesha wanafunzi kukua, kujifunza, na kustawikatika mazingira salama na yenye afya skuli.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mgeni Rasmi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Muhamed Mussa, amesisitiza umuhimu wa kuwa na takwimu za kuaminika ili kuchagiza afua madhubuti za afya skuli.
Aidha, vitabu vya hadithi vilivyo kabidhiwa leo vimetengenezwa kusaidia utoajiwa elimu ya msingi ya afya na ustawi skuli kwa kutoa nyenzo zinazovutia, zinazofaa kwa umri wa wanafunzi, na zinazohimiza tabia chanya pamoja na stadiza maisha miongoni mwa wanafunzi wa skuli za msingi.
UNESCO, kupitia Mkuu wake wa ofisi na mwakilishi mkazi Bw. Michel Toto, imeeleza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wa maendeleo katika kuboresha afya na ustawi wa watoto na vijana Zanzibar.
Kwa kuimarisha mifumo ya data na kutoa nyenzo za kujifunzia , mpango huu unachangia kuhakikisha kuwa skuli hazibaki kuwa sehemu za kujifunzia pekee, bali pia ni mazingira yanayokuza ustawi wa kimwili, kiakili, na kijamii kwa wanafunzi.



0 Comments