
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Bw. Leo Komba ametoa wito kwa wawekezaji pamoja na wananchi kuhakikisha wanalipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kuendelea kuboresha huduma za kijamii na maendeleo ya wananchi.
Wito huo ameutoa wakati wa ziara ya kutembelea eneo moja la uwekezaji lililoachwa bila kuendelezwa na mwekezaji wake, ambapo alisisitiza kuwa maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji yanapaswa kuendelezwa kwa mujibu wa masharti na sheria za ardhi nchini.
Amesema Serikali itaendelea kuwafuatilia wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi pamoja na kuhakikisha maeneo yote ya uwekezaji yanatumika kama ilivyokusudiwa ili kuongeza tija ya kiuchumi kwa Mkoa wa Shinyanga na Taifa kwa ujumla.
Ziara hiyo ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya pango la ardhi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutekeleza wajibu wao wa kisheria katika matumizi sahihi ya ardhi.










0 Comments