Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWAAPISHA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amewaapisha Majaji wa Mahakama Kuu aliowateua hivi karibuni kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya uapisho huo, Rais Dkt. Samia amewataka Majaji hao kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwajibikaji na uzalendo, kwa kutambua wajibu na uzito wa dhamana waliyopewa ya kusimamia haki za wananchi na maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, uteuzi wa Majaji katika ngazi hiyo ya juu ya Mahakama ni sehemu ya hatua za kuimarisha mfumo wa utoaji haki nchini, ikiwemo kukabiliana na ongezeko la mashauri na mahitaji ya wananchi.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amesema Serikali itaendelea kuiwezesha
Mahakama ili kuongeza ufanisi katika utoaji haki na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kimahakama kwa wakati.

Aidha, Rais Dkt. Samia amewataka Majaji hao kuzingatia maadili ya kazi, nidhamu na busara katika maamuzi yao, ili kuendelea kulinda hadhi ya Mahakama na imani ya umma kwa Mhimili huo.

Majaji walioapishwa ni Mhe. Imani Daud Aboud, Mhe. Rabia Hussein Mohamed, Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina, Mhe. Immaculata Kajetan Banzi, Mhe. Cyprian Phocas Mkeha, Mhe. Yohane Bokobora Masara, Mhe. Dkt. Juliana Laurent Masabo, Mhe. Abdi Shaaban Kagomba, na Mhe. Mzee Ibrahim Ibrahim.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Imani Daud Aboud kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Rabia Hussein Mohamed kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Immaculata Kajetan Banzi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Cyprian Phocas Mkeha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Yohane Bokobora Masara kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Juliana Laurent Masabo kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Abdi Shaaban Kagomba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiapa Kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Majaji 9 wa Mahakama ya Rufani, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha na Majaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Uapisho wa Majaji 9 wa Mahakama ya Rufani, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Mei, 2026.

Post a Comment

0 Comments