Ticker

6/recent/ticker-posts

CHEREHANI AZINDUA SHULE YA SEKONDARI KIDATO CHA TANO NA SITA SABASABINI - USHETU

 

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akikagua moja ya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Sabasabini.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini (Kidato cha Tano na Sita) iliyopo Kata ya Sabasabini, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu. 
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani (aliyevaa miwani), akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini, uliofikia hatua za mwisho za ukamilishaji na unatarajiwa kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu ya sekondari.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog, Ushetu

Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, amezindua rasmi Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini (Kidato cha Tano na Sita) iliyopo Kata ya Sabasabini, huku akiipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha sekta ya elimu na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo ya vijijini.

Uzinduzi huo uliofanyika Juni 14, 2026, umefungua ukurasa mpya wa maendeleo ya elimu katika Kata ya Sabasabini baada ya shule hiyo kupangiwa wanafunzi 104 wa Kidato cha Tano watakaoanza masomo mwezi Julai mwaka huu.


Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali, chama, wazazi na wananchi, Mhe. Cherehani alisema maendeleo yanayoonekana leo katika Jimbo la Ushetu ni matokeo ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kupeleka huduma muhimu karibu na wananchi.

Amesema hatua ya Shule ya Sekondari Sabasabini kuanza kutoa elimu ya Kidato cha Tano na Sita ni ushahidi wa namna serikali inavyoendelea kuwekeza katika elimu ili kuhakikisha vijana wa maeneo ya vijijini wanapata fursa sawa za masomo bila kulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta shule za sekondari ya juu.
Mbunge wa Ushetu Mhe. Emmanuel Peter Cherehani akitembelea majengo ya madarasa na miundombinu mingine katika Shule ya Sekondari ya Sabasabini mara baada ya kuzindua rasmi shule hiyo iliyopandishwa hadhi kuanza kutoa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.

"Shule hii imekamilika kutokana na maamuzi makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita. Mhe. Rais Samia hana makeke, anatekeleza. Fedha nyingi zimeendelea kutolewa kwa ajili ya shule, barabara, maji na miradi mingine ya maendeleo. Haya ndiyo matokeo tunayoyaona leo hapa Sabasabini," amesema Mhe. Cherehani.

Mbunge huyo amesema serikali imeendelea kuwekeza fedha nyingi katika sekta ya elimu kwa kujenga shule mpya, madarasa, mabweni na nyumba za walimu, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi nchini.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu ndani ya Jimbo la Ushetu, Mhe. Cherehani amesema katika kipindi cha miaka minne ya ubunge wake amefanikiwa kusimamia ujenzi na ukamilishaji wa shule tatu za sekondari za juu (High Schools), hatua iliyoongeza fursa za elimu kwa vijana wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akikagua moja ya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Sabasabini.

Amezitaja shule hizo kuwa ni Shule ya Sekondari ya Juu Mweli, Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini na Shule ya Sekondari ya Juu Dakama, ambazo sasa zinatoa fursa kwa wanafunzi kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano na Sita karibu na maeneo wanayoishi.

"Katika kipindi cha miaka minne tumefanikiwa kukamilisha shule tatu za sekondari za juu ndani ya Jimbo la Ushetu. Haya ni mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na yanaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kusogeza huduma za elimu karibu na wananchi," amesema Cherehani.

Aidha, amesema Jimbo la Ushetu limeendelea kunufaika na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo maji, afya, umeme na barabara ambayo imekuwa chachu ya ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

Kuhusu changamoto ya maji katika shule hiyo, Cherehani amesema yupo tayari kushirikiana na serikali kuhakikisha kisima kinachimbwa ili kutoa huduma ya uhakika kwa wanafunzi na walimu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani.

"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuletea gari la kuchimba visima mkoani Shinyanga. Mimi nitalipia gharama za vifaa vitakavyohitajika ili kisima kipatikane. Tunataka maji yafike hadi mabwenini ili wanafunzi wapate mazingira bora ya kujifunzia," amesema.

Amewataka pia wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kutumia fursa zilizopo kujiongezea kipato na kuimarisha uchumi wa familia zao.

"Miradi mnayoiona leo imetekelezwa kwa fedha za serikali. Tuitumie fursa hii kufanya kazi kwa bidii, kulima na kuwekeza ili kuinua maisha ya familia zetu na jamii kwa ujumla," amesisitiza.

Mbunge huyo pia amewataka wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano walimu na kuwalinda ili waweze kutekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri na yenye utulivu.

Zaidi ya Shilingi Milioni 617 Zawekezwa Shuleni

Akitoa taarifa ya shule, Mkuu wa Shule ya Sekondari Sabasabini, Yona Zebedayo Mtinda, amesema shule hiyo imepata mafanikio makubwa ya miundombinu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kutokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika sekta ya elimu.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Sabasabini, Yona Zebedayo Mtinda.

Amesema shule imepokea jumla ya Shilingi milioni 617.4 zilizotumika kujenga madarasa, vyoo pamoja na bweni la wavulana, hatua iliyowezesha kupanuka kwa miundombinu na hatimaye kupandishwa hadhi kuwa shule ya sekondari ya juu.

Mtinda amesema mwaka wa fedha 2022/2023 shule ilipokea Shilingi milioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, huku mwaka wa fedha 2024/2025 ikipokea Shilingi milioni 159 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa ya Kidato cha Tano na Sita.

Aidha, Shilingi milioni 248.4 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa pamoja na matundu manane ya vyoo, huku Shilingi milioni 90 zikielekezwa katika ujenzi wa bweni la wavulana kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

"Leo tunajivunia kuwa shule yetu imepanda hadhi na imepangiwa wanafunzi 104 wa Kidato cha Tano watakaoanza masomo mwezi Julai mwaka huu. Hii ni hatua kubwa katika historia ya shule yetu na Kata ya Sabasabini kwa ujumla," amesema Mtinda.

Ameongeza kuwa bweni la wavulana lililogharimu Shilingi milioni 90 limefikia hatua za mwisho za ukamilishaji, ambapo zaidi ya Shilingi milioni 87.4 tayari zimetumika katika utekelezaji wa mradi huo.

Hata hivyo, amesema bado shule inahitaji nyumba za walimu pamoja na kisima cha maji ili kuboresha zaidi mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Mtinda ametoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani na Diwani wa Kata ya Sabasabini Mhe. Emmanuel Makashi kwa mchango wao mkubwa ulioiwezesha shule hiyo kufikia hatua ya kuanza kutoa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.

CCM Yasema Ushetu Ni Mfano wa Maendeleo

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga, amesema maendeleo yanayoonekana katika Jimbo la Ushetu ni matokeo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na viongozi wanaowajibika kwa wananchi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga.

"Hakuna chama kitakachofanya maendeleo makubwa zaidi ya CCM kwa sababu sisi tunatekeleza ilani. Mhe. Cherehani anawajibika kwa wananchi wake na matokeo ya kazi yake yanaonekana wazi. Ana kasi kubwa ya maendeleo," amesema Chatwanga.

Ameongeza kuwa Ushetu imeendelea kuwa mfano wa amani, mshikamano na maendeleo huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi wao kwa ajili ya ustawi wa eneo hilo.

 Chatwanga pia amewataka viongozi wote wanaotokana na CCM kuanzia Mabalozi wa Nyumba Kumi, Wenyeviti, Madiwani na Wabunge kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi kwa vitendo.

Makashi na Magema Wampongeza Cherehani

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Sabasabini, Emmanuel Makashi, amempongeza Mbunge Cherehani kwa mchango wake mkubwa katika kuharakisha maendeleo ya kata hiyo.
Diwani wa Kata ya Sabasabini, Mhe. Emmanuel Makashi.

Amesema wananchi wa Sabasabini wameendelea kunufaika na maboresho ya huduma za elimu, afya na maji, huku akimuomba mbunge huyo kusaidia upatikanaji wa kisima cha maji ili kuondoa changamoto inayowakabili wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.

"Mbunge wetu amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Sabasabini. Leo tunajivunia kuwa na shule ya sekondari ya juu, mabweni, madarasa mapya na miradi mingine mingi ya maendeleo inayobadilisha maisha ya wananchi wetu," amesema Makashi.

Naye Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Ushetu na aliyekuwa Meneja wa Kampeni wa mbunge huyo kwenye uchaguzi Mkuu mwaka 2025, Emmanuel Magema, amesema wananchi wa Ushetu walifanya uamuzi sahihi kumchagua Cherehani kutokana na namna anavyotekeleza ahadi zake kwa vitendo.
Emmanuel Magema.

"Mbunge tuliyenaye ni mchapa kazi. Miradi ya elimu, maji, afya na miundombinu inayotekelezwa leo ni ushahidi kuwa wana Ushetu hawakukosea kumchagua. Matokeo ya kazi yake yanaonekana na wananchi ndiyo mashahidi wakubwa," amesema Magema.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka fedha za maendeleo vijijini na kumpongeza Mbunge Cherehani kwa kusikiliza na kutatua changamoto zao.
Wamesema miradi ya shule, mabweni, vituo vya afya, zahanati, huduma za maji na umeme imeendelea kuboresha maisha yao na kuleta matumaini mapya kwa jamii.

Wameongeza kuwa Uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini unaendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kusogeza huduma za elimu karibu na wananchi na kuimarisha maendeleo ya vijijini.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sabasabini wametoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo na kuanzishwa kwa Kidato cha Tano na Sita, hatua ambayo imewapa fursa ya kuendelea na masomo karibu na makazi yao.

Wanafunzi hao pia wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, pamoja na Diwani wa Kata ya Sabasabini, Mhe. Emmanuel Makashi, kwa juhudi zao za kusimamia maendeleo ya elimu katika eneo hilo ambazo zimewezesha shule hiyo kupata Kidato cha Tano na Sita. Sasa wana mazingira bora zaidi ya kujifunzia na kutimiza ndoto zao.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini (Kidato cha Tano na Sita) iliyopo Kata ya Sabasabini, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Viongozi, wananchi na wadau mbalimbali wakipiga makofi kushuhudia uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini (Kidato cha Tano na Sita) katika Kata ya Sabasabini, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani (aliyevaa miwani), akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini, uliofikia hatua za mwisho za ukamilishaji na unatarajiwa kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu ya sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani (aliyevaa miwani), akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini, uliofikia hatua za mwisho za ukamilishaji na unatarajiwa kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu ya sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, (aliyevaa miwani) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini, Yona Zebedayo Mtinda, wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana uliofikia hatua za mwisho za ukamilishaji na unatarajiwa kuboresha mazingira ya malazi kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, (aliyevaa miwani kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini, Yona Zebedayo Mtinda.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani (aliyevaa miwani), akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini, uliofikia hatua za mwisho za ukamilishaji na unatarajiwa kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu ya sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akipiga picha ya pamoja na wananchi, viongozi na wadau mbalimbali mbele ya bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo uliofikia hatua za mwisho za ukamilishaji.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akitoka katika bweni la wavulana mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi huo unaotarajiwa kuhudumia wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini.
Muonekano wa sehemu ya jengo la utawala katika Shule ya Sekondari Sabasabini.
Mbunge wa Ushetu Mhe. Emmanuel Peter Cherehani akitembelea majengo ya madarasa na miundombinu mingine katika Shule ya Sekondari ya Sabasabini mara baada ya kuzindua rasmi shule hiyo iliyopandishwa hadhi kuanza kutoa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akikagua moja ya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Sabasabini.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akiwa ameketi katika moja ya madawati ndani ya darasa la Shule ya Sekondari ya Sabasabini
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akikagua moja ya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Sabasabini.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akizungumza na wananchi wa Kata ya Sabasabini wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari Sabasabini.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akizungumza na wananchi wa Kata ya Sabasabini wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari Sabasabini.

Post a Comment

0 Comments