Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. ABBASI ATOA MAFUNZO YA UJENZI WA CHAPA YA TANZANIA KUELEKEA AFCON 2027

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, ametoa mafunzo kwa watoa huduma katika mnyororo wa thamani wa utalii ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027 ambayo Tanzania itaandaa kwa ushirikiano na Kenya na Uganda.

Katika mafunzo hayo, Dkt. Abbasi alisisitiza umuhimu wa kujenga na kulinda chapa ya Tanzania (Tanzania Brand), akieleza kuwa kila mtoa huduma katika sekta ya utalii ana jukumu la kuwa balozi wa nchi kupitia utoaji wa huduma bora kwa wageni watakaofika nchini wakati wa AFCON 2027.

Alibainisha kuwa ubora wa huduma, ukarimu, weledi na uzingatiaji wa maadili ni mambo muhimu yatakayochangia kuimarisha taswira ya Tanzania kimataifa, kuongeza idadi ya watalii na kufungua fursa zaidi za uwekezaji.

Dkt. Abbasi aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatoa huduma zenye viwango vya juu ili kuacha kumbukumbu chanya kwa wageni na mashabiki watakaotembelea Tanzania wakati wa mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Juni 25, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro.

Post a Comment

0 Comments