Wananchi, wanafunzi, wataalamu, wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajiwa kukutana jijini Mbeya Julai 3, 2026, katika mhadhara maalum wa hadhara utakaolenga kujadili nafasi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mhadhara huo, unaoratibiwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Centre, David Kafulila.
Mhadhara huo unafanyika siku tatu baada ya Tanzania kuanza rasmi utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, iliyoanza Julai 1, 2026, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha mjadala wa kitaifa kuhusu namna ubia kati ya Serikali na sekta binafsi utakavyosaidia kuharakisha maendeleo ya nchi.
Washiriki watapata fursa ya kujadili namna PPP inavyoweza kusaidia kupata rasilimali za kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo, kuboresha miundombinu, kuvutia uwekezaji na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
Aidha, mhadhara huo unatarajiwa kuimarisha uelewa kuhusu mchango wa sekta binafsi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050, kuongeza imani ya wawekezaji na kuzijengea taasisi uwezo wa kushirikiana katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya muda mrefu ya Tanzania.














0 Comments