Na Prosper Makene
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya IPU wamehitimisha kikao chao cha 300 jijini Geneva, Uswizi, tarehe 29-30 Juni 2026, chini ya uongozi wa Dkt. Tulia Ackson, Rais wa IPU.
Kikao hicho cha Kikatiba kimeambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mabunge Duniani, tarehe 30 Juni, ambayo ndiyo tarehe ya kuanzishwa kwa IPU.
Katika ajenda, Kamati ilijadili maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 153 wa IPU utakaofanyika Oktoba jijini Arusha, Tanzania, pamoja na uchaguzi wa Rais mpya atakayemrithi Dkt. Ackson.
Vilevile, kikao kilishuhudia makabidhiano ya Ofisi ya Katibu Mkuu. Bw. Martin Chungong alimkabidhi Balozi Anda Filip “funguo” ya uongozi, kufuatia uchaguzi wake Aprili jijini Istanbul. Balozi Filip alichukua wadhifa rasmi tarehe 1 Julai 2026.
Yeye ni Katibu Mkuu wa 10, Mwanamke wa kwanza, na Mtu wa kwanza kutoka Ulaya Mashariki kuongoza Sekretarieti ya IPU kwa kipindi cha miaka minne.
Bunge la Tanzania linampongeza Balozi Filip na linaahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na IPU.




0 Comments