Ticker

6/recent/ticker-posts

WANNE WAPANDIKIZWA FIGO, 38 WAFANYIWA UPASUAJI WA MISHIPA YA KUCHUJA DAMU MNH-MLOGANZILA

Hospitali ya Taifa Muhimbili–Mloganzila kwa kushirikiana na wataalam kutoka Korea Kusini, imewapandikiza figo wagonjwa wanne na wengine 38 wamefanyiwa upasuaji wa kutengeneza na kurekebisha mishipa ya kuchuja damu katika kambi maalum iliyofanyika Agosti 15–19, 2026.

Tangu huduma hizo zianze kutolewa Muhimbili-Mloganzila mwaka 2023, jumla ya wagonjwa 28 wamepandikizwa figo na wagonjwa 289 wamefanyiwa upasuaji wa kutengeneza na kurekebisha mishipa ya kuchuja damu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Godlove Mfuko, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji, amesema wagonjwa wote wameendelea vizuri na wameruhusiwa kwenda nyumbani.

Dkt. Mfuko amesema mafanikio hayo yameonesha matokeo ya uwekezaji mkubwa uliyofanywa na Serikali katika kuboresha miundombinu ya kutolewa huduma za afya, vifaa tiba vya kisasa pamoja na mafunzo ya wataalam.

Post a Comment

0 Comments