Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

DCEA YAKAMATA TANI 18 ZA DAWA ZA KULEVYA


MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata jumla ya kilogramu 18,078.41 za dawa za kulevya katika operesheni zilizofanyika katika mikoa 14 nchini kati ya Julai na Septemba 2026.

Kamishna Mkuu wa DCEA, Kamishna Aretas Lyimo, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, akieleza kuwa operesheni hizo zilifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Dodoma, Mbeya, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Amesema kiasi hicho kinajumuisha kilogramu 11,504.76 za bangi, kilogramu 6,529.5 za mirungi, kilogramu 44.45 za bangi aina ya skanka na gramu 41.25 za heroin.

Kwa mujibu wa Kamishna Lyimo, watuhumiwa 289 walikamatwa katika operesheni hizo, ambapo 169 wamefikishwa mahakamani na taratibu za kisheria zinaendelea dhidi ya wengine.

Aidha, DCEA ilikamata magari nane, bajaji moja na pikipiki 40 zilizodaiwa kutumika katika shughuli zinazohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Kamishna Lyimo amesema bangi imeendelea kuongoza kwa kiwango cha uzalishaji na ukamataji, huku Morogoro na Tabora zikiongoza kwa kiasi kikubwa.

Mkoani Morogoro, DCEA ilikamata kilogramu 6,299.24 za bangi na kilogramu 226 za mbegu za bangi, wakati Tabora zilikamatwa kilogramu 4,650.86 za bangi pamoja na kilogramu 203 za mbegu za bangi.

Post a Comment

0 Comments