Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

HAKIKISHENI MNATUMIA BiDHAA ZINAZOZALISHWA KWA UTOSHELEVU NA VIWANDA VYA NDANI - WAZIRI KAPINGA

-Azitaka taasisi za sekta binafsi na Masharikiano ya wafanyabiashara kukumbushana misingi ya uendelevu wa Viwanda;

-Awataka wafanyabiashara wazawa kuamini bidhaa zinazozalishwa na wazawa wenzao;

-Mwekezaji kiwanda cha Simama Asema uwekezaji wa Bilioni 14 aliowekeza kuchechemua Ari ya wazawa kwenye uwekezaji

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga amevitaka Viwanda vinavyozalisha bidhaa kwa utoshelevu hapa nchini kuhakikisha vinalinda soko la ndani na kuwataka wazawa kuamini bidhaa zinazozalishwa na wazawa wenzao

Mhe Kapinga ameyasema hayo Leo 23 Septemba, 2026 Jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizindua kiwanda cha kutengeneza vizibo cha Simama metal crown kilichoko wilaya ya Kigamboni ambacho kinamilikiwa na mwekezaji mzawa kwa asilimia Mia moja.

Amezitaka taasisi za sekta binafsi Kama CTI, TPSF na TNBC kuhakikisha zinasimamia vema wamiliki wa viwanda na kuwakumbusha misingi waliyojiwekea ya uendelevu wa viwanda.

Ameongeza kuwa bilioni 14 zilizowekezwa kwenye kiwanda hicho ni sehemu ya juhudi za kuongeza uzalishaji wa bidhaa nchini na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje nakuongeza kuwa Serikali itaendelea kuhimiza umuhimu wa uwekezaji kwa wazawa na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Simama Tanzania Bwana Norbert Simama amesema kiwanda hicho cha vizibo kina uwezo wa kuzalisha visoda milioni 130 kwa mwezi kwa ajili ya matumizi ya viwanda vya vinywaji na kwa bora wa kimataifa na kumudu ushindani kimataifa..

Amesisitiza umuhimu wa viwanda vya vinywaji kushirikiana na kiwanda hicho kwa kutumia bidhaa zake, huku akibainisha kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini zinapaswa kuwa bora na kukidhi viwango vinavyohitajika ili kuongeza ushindani na kuimarisha soko la ndani.

Aidha, amesema mipango ya maendeleo ya viwanda inahitaji ushiriki wa sekta binafsi, huku Serikali ikiendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji, akieleza kuwa kufikia uchumi wa dola trilioni moja kunategemea kwa kiasi kikubwa uwekezaji katika sekta ya viwanda.

Ametoa wito kwa wadau kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutimiza vigezo vya ubora ili kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za ndani na kukuza uchumi wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments