Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

BARAZA LA WAFANYAKAZI TEA LAPITIA MPANGO MKAKATI WA TANO

MOROGORO

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamepitia na kujadili Mpango Mkakati wa Tano wa Mamlaka hiyo (2026/27–2030/31), pamoja na kutathmini utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Nne (2021/22–2025/26).

Akizungumza katika Kikao cha Pili cha Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa TEA, Mwenyekiti wa Baraza ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha, amesisitiza umuhimu wa maoni na ushiriki wa wajumbe katika kuboresha mpango huo ili kuhakikisha vipaumbele na malengo ya Mamlaka yanafikiwa kwa ufanisi.

Mpango Mkakati wa Tano umezingatia miongozo muhimu ya maendeleo ya Taifa, ikiwemo Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2023 pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Katika kikao hicho kilichofanyika Morogoro, Novemba 2–3, 2026, wajumbe pia walipokea na kujadili taarifa ya mapitio ya Sheria ya Mfuko wa Elimu ya mwaka 2001 inayolenga kuimarisha utendaji na ufanisi wa Mamlaka.

Post a Comment

0 Comments