Ticker

6/recent/ticker-posts

RC GABRIEL AZITAKA TAASISI NA MASHIRIKA KUSHIRIKANA NA HESLB


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert akiwasili na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru wakati alipofika kufungua Kikao Kazi cha 10 cha Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu leo Jumatatu (Oktoba 10, 2021) leo Jijini Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert akiwasili na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru wakati alipofika kufungua Kikao Kazi cha 10 cha Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu leo Jumatatu (Oktoba 10, 2021) leo Jijini Mwanza.

Baadhi ya Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi wa kikao kazi cha 10 cha Maafisa hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo Jumatatu (Oktoba 10, 2021) Jijini Mwanza.

Baadhi ya Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi wa kikao kazi cha 10 cha Maafisa hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo Jumatatu (Oktoba 10, 2021) Jijini Mwanza.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi wa kikao kazi cha 10 cha Maafisa hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo Jumatatu (Oktoba 10, 2021) Jijini Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akionesha kwa waandishi wa habari, Mwongozo kuhusu utaratibu wa malipo mbalimbali ya wanafunzi wakati wa ufunguzi wa kazi kazi cha 10 cha Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu leo Jumatatu (Oktoba 11, 2021).

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akimkabidhi Tuzo ya Afisa Mikopo bora katika usimamizi wa Madawati ya Mikopo ya Taasisi za Elimu ya Juu, Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Salmon Daud wakati wa wa ufunguzi wa kazi kazi cha 10 cha Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu leo Jumatatu (Oktoba 11, 2021).

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akimkabidhi Tuzo ya Afisa Mikopo bora katika usimamizi wa Madawati ya Mikopo ya Taasisi za Elimu ya Juu, Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Goldon Chavala wakati wa wa ufunguzi wa kazi kazi cha 10 cha Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu leo Jumatatu (Oktoba 11, 2021).

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akimkabidhi Tuzo ya Afisa Mikopo bora katika usimamizi wa Madawati ya Mikopo ya Taasisi za Elimu ya Juu, Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Lugano wakati wa ufunguzi wa kazi kazi cha 10 cha Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu leo Jumatatu (Oktoba 11, 2021).

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akionesha tuzo ya kutambua mchango wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo katika kuiwezesha HESLB kutekeleza majukumu yake ya kisheria wakati wa ufunguzi wa kazi kazi cha 10 cha Maafisa Madawati ya Mikopo katika Taasisi za Elimu ya Juu leo Jumatatu (Oktoba 11, 2021).

(PICHA NA HESLB)

***********************************

Na Mwandishi Wetu,

HESLB,

Mwanza

11.10.2021



MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amezitaka taasisi, mashirika na makampuni ya sekta za umma na binafsi kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) katika kuwabaini wanufaika wa mikopo hiyo ili kuiwezesha Serikali kuwa na mfuko endelevu wa elimu ya juu.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kikao kazi cha 10 cha Maafisa Madawati ya Mikopo katika taasisi za Elimu ya Juu kinachoendelea Jijini Mwanza leo Jumatatu Oktoba 11, 2021, Mhandisi Gabriel alisema ni wajibu wa wanufaika kurejesha mikopo hiyo, kwani HESLB imewawezesha kupata ujuzi wa kitaaluma na kuweza kujiinua kiuchumi kupitia Elimu.

“Tunatambua kuna idadi kubwa ya wataalamu waliowezeshwa na HESLB kupata mikopo ya elimu ya juu, ni wajibu wetu kuhakikisha tunarejesha fedha hizo ili ziweze kuwanufaisha Watanzania wahitaji, Ofisi yangu itashirikiana na HESLB katika kuhakikisha wanufaika waliopo katika sekta rasmi na zisizo rasmi wanarejesha mikopo hii” alisema Mhandisi Gabriel.

Aidha Mhandisi Gabriel aliitaka HESLB kutumia fursa za majukwaa, mikutano na makongamano ya wadau na wanataaluma mbalimbali ili kuweza kuwabaini wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, kwa kuwa hatua hiyo itaongeza kasi ya makusanyo kutoka kwa wanufaika ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao.

Kwa mujibu wa Mhandisi Gabriel, alibainisha kuwa Mkoa wa Mwanza umekuwa kimbilio kubwa la mikutano na makongamano ya wanataaluma mbalimbali, hivyo HESLB haina budi kuweka mikakati mahsusi ya kupata orodha ya wanufaika walioajiriwa katika makampuni, taasisi na mashirika hayo ili kuweza kuwabaini wanufaika wengi zaisi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema HESLB kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2016/2017-2020/2021), imeendelea kuimarisha mashirikiano na wadau na kubuni mifumo mbalimbali ya urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wanufaika.

“Hivi karibuni tunatarajia kuzindua akaunti ya LIPA, ni akaunti maalum ya mnufaika wa mikopo, kupitia akaunti hiyo mnufaika ataweza kupata taarifa za deni la mkopo aliopatiwa na HESLB wakati wa masomo, hii itaongeza hamasa ya urejeshaji kutoka kwa wanufaika” alisema Badru.

Akizungumzia maudhui ya kikao kazi hicho, Badru alisema kikao hicho kimeshirikisha jumla ya washiriki 150 kutoka taasisi za elimu ya juu 81 za umma na binafsi, wakiwemo Maafisa Mikopo takribani 125; wawakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Menejimenti ya HESLB.

“Maafisa Mikopo ni wadau muhimu wa HESLB, kutokana na majukumu yenu ya kuhudumia wanafunzi tumeamua kukutana nanyi ili kubadilishana uzoefu katika eneo la upangaji, utoaji na urejeshaji mikopo lakini pia kupokea maoni, ushauri na changamoto katika sehemu za kazi” alisema Badru.

Naye Meneja wa HESLB, Kanda ya Ziwa, Usama Choka alisema Ofisi yake imeendelea kupata ushirikiano mkubwa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mwanza katika juhudi na jitihada mbalimbali inazoendelea kuzifanya katika kuwabaini wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Post a Comment

0 Comments