Ticker

6/recent/ticker-posts

MIRADI YA UBIA KATI YA SEKTA BINAFSI NA UMMA YAWAKOSHA WANANCHI


Mtaalamu wa Masuala ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Kalokola Osward, akitoa elimu kuhusu alama za noti halali, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Mtaalamu wa masuala ya mfumo ya kielektroniki ya malipo ya Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dominic Kounja, akitoa elimu ya mfumo huo kwa mkazi wa Dar es Salaam, Bi. Sylivia Kilarika, alipotembelea Banda la Wizara hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Mtaalamu wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Isaac Wilson, akitoa elimu ya Sera za Huduma za Fedha kwa mkazi wa Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Mtaalamu wa Uchambuzi wa masuala ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Gloria Chellunga, akitoa elimu ya mikopo kwa wakazi wa Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Mtaalamu wa Miradi ya Ubia kati ya Sekta binafsi na umma (PPP), Bw. Edwin Kachenje, akielezea utaratibu wa kufanya miradi ya PPP, kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

Post a Comment

0 Comments