Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA WAHAMASISHWA KUCHANGIA DAMU SALAMA KUOKOA MAISHA

Mkurugenzi wa Chou cha Hermargs na Mlezi wa Rotaract SUA Profesa Robinson Mdegela akitoa neno kwa vijana hao walioshiriki kwenye zoezi la uchangiaji wa Damu kabla ya zoezi hilo kuanza wakati wa kutoa umuhimu wa uchngiaji wa damu.
Mkuu wa Chuo cha Afya Hermargs ambao ni wenyeji wa zoezi hilo Benedict Lubusha akitoa neno la ukaribisho na shukrani kwa vijana hao.
Vijana kutoka Rotaract SUA na Hermargs wakichanga damu salama.
Picha namba 9 havijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa k


Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.
Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.
Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.
Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.

Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.

***************
Na: Amina Hezron,Morogoro.


KWAKUTAMBUA uhitaji nmkubwa wa dam hasa kwa mkoa wa Morogoro Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) na Chuo cha Afya Hermargs ambao ni wanachama Rotaract wameungana kuchangia damu ili iweze kusaidia kupunguza uhitaji mkubwa wa dam una kusaidia jamii na watu wenye uhitaji.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mlezi wa kikundi cha Rotaract SUA Profesa Robinson Mdegela amesema kuwa mkoa wa Morogoro ni moja ya mikoa mbayo imekuwa ikipokea majuruhi na watu wengi pale zinapotokea ajali kutokana na kuwa katikati na kuunganisha safari za Dar Mwanza,Dar Mbeya na mikoa mingine hivyo kumekuwa na uhitaji mkubwa sana damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

“Wamefanya kazi nzuri ambayo ni mbegu ya kuzidi kuhamasishana na kusaidiana ili changamoto ya ukosefu wa damu isiendelee kuwepo na vijana Wetu hawa wanawajibu wa kufanya changizo kama walivyofanya siku ya leo ili iwe chachu kwa jamii na vijana wengine lakini pia kutoa mchango wao kwa jamii “, alisema Profesa Mdegela.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Afya Hermargs ambao ni wenyeji wa zoezi hilo Benedict Lubusha amewashukuru walezi wa vikundi vyote ambavyo vimewezesha kufanyika kwa zoezi zima la uchangiaji wa damu salama itakayosaidia kuokoa maisha ya makundi maalum.
“Tunajua kuwa kila siku ajari zinatokea na tunajua kuwa hakuna sehemu duniani kuna kiwanda cha damu lakini hii damu inatoka kwa binadamu kwahiyo na sisi leo tumefanya uchangiaji wa damu kwaajili ya wenzetu ambao wanauhitaji wa damu”, alisema Lubasha.

Aliongeza “Ukiangalia kwa Mkoa wa Morogoro vyuo vipo vingi ukichukua kwa haraka haraka jumla tunapata wanafunzi zaidi ya elfu ishirini kwa mfano tukiweza kupata wanafunzi nusu ya hao wakachangia damu tutakuwa tumelisaidia taifa kwakiasi kikubwa kwakuwa huwezi jua lini na wewe utakuwa na uhitaji wa damu”.

Naye mmoja ya wanafunzi waliojitokeza kuchangia damu kutoka SUA, Khatibu Mgunya amewataka vijana kuwa na moyo wa kujitolea kwa kujijengea mazoea ya kwenda kuchangia damu mara kwa mara ili kuepusha vifo vya watoto na wajawazito vinavyotokana na kukosekana kwa damu.

Naye Mwanafunzi wa kazi ya ufamasia Katika chuo cha Hermargs Agneta Lwebangila amewataka vijana wengine kujitokeza kuchangia damu kwakuwa itasaidia kuokoa maisha ya wengine.

“Kuna watu wanaogopa kuchangia damu wakidhani kufanya hivyo kuna madhara yeyote si kweli mimi leo ni mara yangu ya kwanza kuchangia damu na sijapata madhara yeyote nipo salama kabisa hivyo wasiogope tuungane kwa pamoja tuokoe maisha ya wengine kupitia kuwasaidia damu salama”, alisema Agneta.

Kwa upande wake muuguzi na Mratibu wa kitengo cha damu salama kutoka Katika kitengo cha Hospital ya rufaa Mkoa Morogoro Vaileth Mrija amewataka wananchi kuhamasika kuchangia damu ili kuokoa pia maisha ya watoto ambao wa matatizo ya Cell mundu pamoja na magonjwa ya Kansa ambao nao wamekuwa na uhitaji mkubwa wa damu.

“Maahitaji ya Damu kwa siku kwenye hospitali yetu ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ni wastani wa zaidi ya chupa 23 hivyo unaweza kuona uhitaji ulivyo mkubwa na pale kwa bahati mbaya zinapotokea ajali uhitaji huwa mkubwa zaidi kulingana na tatizo lenyewe hivyo tunashukuru vijana hawa kwa kuamua kuchangia damu” alisema Bi Mrija.

Post a Comment

0 Comments