Ticker

6/recent/ticker-posts

Vijana wahamasishwa kuwekeza kwenye ufagaji wa kuku

Na Mwandishi Wetu

Wafugaji wa kuku nchini wamehimizwa kutumia chakula bora cha mifugo ili kuongeza uzalishaji, kuboresha afya ya kuku na kuongeza faida ya biashara zao, huku vijana wakitakiwa kuchangamkia fursa za ufugaji wa kuku kama njia ya kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Wito huo unakuja sambamba na upanuzi wa huduma za kampuni ya Ekama Animal Feeds ambayo imefungua rasmi tawi jipya la Gongolamboto, Dar es Salaam, litakaloanza kutoa huduma kuanzia Julai 1, 2026 kwa lengo la kuwasogezea wafugaji bidhaa na huduma za kitaalamu.

Kupitia tawi hilo jipya lililopo eneo la Mombasa-Gongolamboto, wafugaji watapata huduma za ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari wa mifugo bila malipo pamoja na huduma za usafiri bure, hatua inayolenga kupunguza gharama na kuwawezesha kupata huduma kwa urahisi.

Akizungumza na Wadau wa sekta ya mifugo,Meneja mauzo kutoka kampuni ya Ekama Animal Feeds Irene Temba amesema matumizi ya chakula bora ni msingi wa mafanikio katika ufugaji wa kuku kwani huchangia kuku kukua kwa haraka, kuongeza uzalishaji wa mayai na kupunguza magonjwa yanayoweza kuathiri biashara ya mfugaji.

Aidha, amesema kuwa vijana wengi wana nafasi kubwa ya kufanikiwa kupitia ufugaji wa kuku kutokana na ongezeko la mahitaji ya nyama na mayai nchini, hivyo wanapaswa kutumia fursa hiyo kwa kuanzisha miradi ya kisasa yenye kuzingatia matumizi ya lishe bora kwa mifugo.

Imeelezwa kuwa sekta ya ufugaji inaweza kuwa chanzo kikubwa cha ajira na kipato kwa vijana ikiwa watawekeza katika elimu ya ufugaji, matumizi ya teknolojia na bidhaa zenye ubora zinazowezesha kupata mavuno yenye tija.

Ekama Animal Feeds imeendelea kusambaza chakula cha kuku katika maeneo mbalimbali ikiwemo Bagamoyo, Kimara Suka, Zanzibar, Kongowe na sasa Gongolamboto, hatua inayoongeza upatikanaji wa bidhaa zake kwa wafugaji wa maeneo mbalimbali.

Ufunguzi wa tawi hilo jipya unatarajiwa kuimarisha huduma kwa wafugaji wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani, huku ukiwa chachu ya kuhamasisha vijana wengi zaidi kuingia kwenye ufugaji wa kuku kama biashara yenye uwezo wa kuchangia ukuaji wa uchumi wa mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments