Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA ELIMU YATAKIWA KUENDELEA KUFANYA MAPITIO YA SERA YA ELIMU YA 2014 KUBADILISHA MITAALA, KUONGEZA UBORA WA ELIMU NA MAFUNZO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitembelea na kupata maelezo katika mabanda mbalimbali ya taasisi za serikali na binafsi zinazojihusisha na ubunifu na utafiti wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa mbunifu wa gari linalotumia umeme Masoud Kipanya wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 ambayo yaliandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza mtoto Ethan Kaganda aliyebuni mfumo wa kutoa taarifa iwapo wanafunzi zaidi ya mmoja wameingia katika choo kimoja kwa wakati mmoja ili kuepusha wenye nia ovo wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 ambayo yaliandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza mtoto Tanya Gorecha aliyebuni aliyebuni mifumo mbalimbali ya umeme wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 ambayo yaliandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisiliza maelezo kutoka kwa meneja wa Funguo Innovation kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Joseph Manirakiza wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 ambayo yaliandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na washiriki pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 ambayo yaliandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimkabidhi hundi ya shilingi milioni tano mshindi wa ubunifu Arqhm Isihaka Adam kutoka Shule ya Msingi Mikumi Mpya Morogoro aliyebuni kengele ya nyumbani inayotumia sauti na mwanga kwaajili ya watu wote ikiwemo wenye mahitaji maalum wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 19 Mei 2022. Kushoto ni Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, kulia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wabunifu waliotwaa tuzo wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 ambayo yaliandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. ............................................ Na Zena Mohamed,Dodoma. MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,ameiagiza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuhakikisha inaendelea kujenga mazingira rafiki yatakayowezesha wanafunzi kupenda zaidi kusoma masomo ya sayansi na teknolojia. Pamoja na kuendelea kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na kubadilisha mitaala ili kuongeza ubora wa elimu na mafunzo. Dkt.Mpango ameyasema hayo jijini hapa leo wakati akifunga maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO. "Naiagiza Wizara ya Elimu kuendelea kutafuta fursa za masomo kwa kwa watanzania katika vyuo bora duniani katika nyanja za sayansi, teknolojia na tiba kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020,"amesema Dkt.Mpango. Amesema Wizara inapaswa kuwafuatilia kwa karibu wanafunzi wabunifu na kuhakikisha wanaendelezwa ili waweze kuwa msaada katika utatuzi wa changamoto mbalimbali kwa kutumia teknolojia,"amesema Dk.Mpango. Pia amewataka watanzania kuwa na desturi ya kununua na kutumia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na watanzania ili kukuza mnyororo wa ndani ya nchi. "Ndugu zangu watanzania niwasihi tu mhakikishe mnapenda na kuthamini vyakwetu,tuwe na utamaduni wa kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini kwetu na watanzania wenzetu,"amesema. Hata hivyo amesema kuwa familia pia zina wajibu wa kuwahamasisha na kuwatia moyo watoto wanapokuwa na mawazo ya kibunifu pamoja na kuwaunga mkono katika kupenda elimu ya sayansi na kusema kuwa mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yanapaswa kufanyika katika mikoa yote nchini. Pamoja na hayo pia ameiagiza Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhakikisha Halmashauri zinatenga maeneo maalum ya kuanzisha vituo vya ubunifu na atamizi za kisekta kulingana na shughuli za kiuchumi katika maeneo husika kwa ajili ya kulea vijana wenye ubunifu, ugunduzi na maarifa asilia. Sambamba na hayo Makamu wa Rais ameitaka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kuhamisha maarifa ya tafiti katika vitendo pamoja na kuendelea kutambua mazao yanayoweza kuwasaidia wakulima hasa wale wa chini kwa urahisi zaidi kulingana na mvua zinazopatikana katika mkoa husika. Kwa Upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa dhati kuwahudumia wabunifu ili mawazo na ubunifu uweze kutumika na jamii ya watanzania. Pia amezitaka taasisi zinazohudumia wabunifu kujipanga na kutoa elimu kwa wabunifu ili waweze kupata uhakika wa kile wananchobuni ikiwa nikuendelea kutambua kuwa bunifu wanazotengeneza ni Mali zao na sio za mtu mwingine pamoja na kulinda na kupata haki zao za msingi. Awali Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika maadhimisho hayo amesema serikali kupitia Buni Hub na DTBI imewezesha kuanzishwa kwa makampuni zaidi ya 94 yaliotokana na ubunifu na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 30000. Aidha Prof Mkenda amesema mchango wa kampuni hizo katika pato la taifa umeanza kuonekana kutoka na baadhi ya kampuni hizo kuchangia zaidi milioni 500 kwa mwaka kila mmoja.

Post a Comment

0 Comments