Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. MWIGULU NCHEMBA ASHIRIKI UFUNGUZI WA BARABARA YA EAC ARUSHA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw. Daniel Chongolo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya mchepuko ya Kikanda, ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass), iliyofunguliwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Wakuu wa Mikoa ya Tanga, Bw. Adam malima (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Stephen Kagaigai (katikati), wakati wa Hafla ya Ufunguzi wa Barabara ya Mchepuko ya Kikanda, ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass), ikiwa ni sehemu ya mradi wa kuboresha miundombinu ya barabara ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kuhitimishwa kwa hafla ya ufunguzi wa barabara ya mchepuko ya Kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass), iliyozinduliwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Bw. Shaka Hamdu Shaka, wakati wa hafla ya ufunguzi wa barabara ya mchepuko (Arusha Bypass) ambayo ni barabara ya Kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliyozinduliwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo, Jijini Arusha

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa ameshikilia Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa kuwaaga Marais na Viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, walioshiriki hafla ya uzinduzi wa barabara ya Kikanda ya mchepuko (Arusha Bypass), iliyozinduliwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha. Kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi, wakimpungia mikono Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (Hayupo pichani) wakati akiondoka katika eneo la Ufunguzi wa Barabara ya Afrika Mashariki ya mchepuko (Arusha Bypass), iliyofunguliwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo, Jijini Arusha.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Arusha)

Post a Comment

0 Comments