Ticker

6/recent/ticker-posts

MAAFISA ARDHI MKOA WA SINGIDA WATAKIWA KWENDA KUTOA USHAHIDI BARAZA LA ARDHI

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza kwenye kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi mkoa kilichofanyika mjini hapa leo Julai 22, 2022 katika Ukumbi wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG). Kushoto ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza.
Afisa Utumishi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Salum Issa akizungumza kwenye kikao hicho.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza. akiongoza kikao hicho.


Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Singida, Bahati Colex akizungumza kwenye kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi mkoa kilichofanyika mjini hapa leo Julai 22, 2022 katika Ukumbi wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
Maafisa Ardhi wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Mpima ardhi Mkoa wa Singida, Sesaria Martin akichangia jambo kwenye kikao hicho
Afisa Mipangomiji Manispaa ya Singida, Aristides Mulokozi akitoa taarifa ya utendaji kazi.
Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ibrahim Magesa akitoa taarifa kwenye kikao hicho.
Afisa Ardhi Wilaya ya Ikungi, Ambross Ngonyani akitoa taarifa.


Afisa Ardhi wa Wilaya ya Itigi, Mfwimi Abraham akitoa taarifa.
Afisa Ardhi Msaidizi Wilaya ya Manyoni, Aron Bisama akitoa taarifaya ufanyaji kazi.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MAAFISA Ardhi katika Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Singida wametakiwa kwenda kutoa ushahidi kwenye baraza la usuluhishi wa migogoro ya ardhi baada ya kupeleke kesi mbalimbali ili kuzipa msukumo wa kusikilizwa na kumalizwa.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Singida, Bahati Colex kwenye kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi mkoa kilichofanyika mjini hapa leo Julai 22, 2022 katika Ukumbi wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

"Kumekuwa na changamoto kubwa ya maafisa ardhi kushindwa kuja kwenye mabaraza ya usuluhishi kutoa ushahidi wa kesi mbalimbali jambo ambalo linachangia kuwepo kwa kesi nyingi ambazo haziendelei kutokana na kukosekana kwa ushahidi na kusababisha walalamikaji kukosa haki" alisema.

Afisa Utumishi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Salum Issa akizungumza na maafisa ardhi hao aliwaomba watumishi wote wa wizara hiyo kupeleka taarifa sahihi za ajira zao na namba za simu jambo litakalowalahisishia kuwatambua na kuwapata kirahisi pale wanapotaka kuwapandisha madaraja na mambo mengine.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko amewapa mwezi mmoja maafisa ardhi hao kuhakikisha wanapima taasisi zote za serikali ili kukabiliana na changamoto ya uvamizi unaofanywa na baadhi ya watu kwenye maeneo yanayomilikiwa na serikali.

"Maafisa ardhi mliopo kwenye halmasauri kapimeni taasisi zote za serikali ili maeneo yote yawe na hati, hivi sasa taasisi nyingi zikiwamo shule zinavamiwa kwasababu hazijapimwa na nyie mpo mnaangalia tu," alisema.

Mwaluko alisema migogoro yote ya ardhi kati ya kijiji na kijiji, wilaya kwa wilaya na Mkoa kwa Mkoa iorodheshwe ifahamike ili hatua za kuipatia ufumbuzi ziweze kuanza haraka .

Aliongeza kuwa migogoro ya ardhi kwenye halmashauri tafsiri itolewe ili iweze kufanyiwa kazi na ile ya mipaka ushauri wa kitaalam utolewe kwani hakuba sababu ya kukaa na migogoro bila kuitafutia ufumbuzi.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza alisema baadhi ya maafisa ardhi wamekuwa kikwazo kutokana na tabia ya kuivaa migogoro badala ya kutoa ushauri.

"Wataalam hatutaki kutoa ushauri wa kuitatua migogoro, tuache tabia ya kuivaa migogoro, tuhakikushe GN zinapatikana," alisema.

Alisema suala la migogoro linafahamika kwa watalaam wote wa ardhi hivyo jukumu lao kubwa ni kutafsiri GN na sio kwenda kueleza wananchi kutafsiri mipaka.

Katika kikao kazi hicho maafisa ardhi wote wa wilaya walipata fursa ya kutoa taarifa za utendaji wa kazi zao ambapo zilijadiliwa ili kuona wapi kulikuwa na upungufu na kuzifanyia kazi lengo likiwa ni kuboresha zaidi utendaji wa kazi na kuondoa kasoro zilizokuwepo.

Post a Comment

0 Comments