Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI SAGINI AWAOMBA WANANCHI WA KIJIJI CHA KEGONGA KUJENGA KITUO CHA POLISI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Jumanne Sagini akizungumza wananchi wa Kijiji cha Kegonga Wilaya ya Tarime Mkoani Mara
Wanakijiji Wakisikiliza Naibu Waziri

*************

NA Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Jumanne Sagini amewaomba wananchi wa Kijiji cha Kegonga Wilaya ya Tarime Mkoani Mara kushirikiana na Serikali kujenga kituo cha polisi Ili kusaidia kuepukana na kero ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma huku Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi itatafuta fedha kusaidia Ujenzi ili ukamilike kwa haraka .

Ombi hilo amelitoa katika ziara yake aliyoambatana na Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe Mwita Waitara ambapo alitembelea na kukagua Kituo cha Polisi Kegonga kilichopo, Kijiji cha Kegonga, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara ili kuangalia kituo hicho kilicholalamikiwa kwenye Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania juu ya ubora wa kituo hicho pamoja na lalamiko la kuhamishwa kwa askari wa kituo hicho.

“Niwasisitize kuwa ni jukumu la kila mwananchi kushiriki katika ulinzi shirikishi siyo kila mnalalamika uhalifu hauishi wakati hamtoi fedha za Ulinzi shirikishi mnazokubaliana kijijini kwenu hivyo mshirikiane na Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime muanze ujezi alafu Wizara kupitia Jeshi la Polisi itajumuika nanyi katika ujenzi wa kituo hicho”amesema Waziri Jumanne.

Hata hivyo Naibu Waziri Sagini amefurahi kukuta askari wa Jeshi la Polisi katika Kituo hicho wanaendelea na majukumu ya kazi na kuwahakikishia wananchi wa Kijiji cha Kegonga kuwa askari wa kituo hicho hawakuhamishwa bali walikuwa kwenye jukumu la kusimamia mitihani .

“Nimefurahi kukuta Askari polisi wapo kituoni,OCS Yussuf yupo pamoja na wasaidizi wake.Na wamesema walikuwa wanasimamia mitihani ndio maana baadhi ya askari hawakuwepo kituoni” amesema Jumanne

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Sagini pia alitembela na kukagua Kikosi cha Polisi Wanamaji Shirati, iliyopo wilayani Rorya ili kufahamu utendaji kazi wao pamoja na changamoto zinazowakabili na kuahidi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itashughulikia changamoto yao ya vifaa vitakavyowasaidi kulinda wavuvi wa Tanzania.

Aidha akitoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri Sagini amewakumbusha wananchi wa Kijiji cha Kegonga kushiriki kwenye Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022 itakayosaidia katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi.

Post a Comment

0 Comments