Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT.HUSSEIN MWINYI AFUNUA TAWI LA BENKI YA CRDB WETE PEMBA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza lac Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika hafla ya ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Wete Pemba leo 25-7-2022, wakati wa ziara yake katika Mkoa huo, kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Mkoa huo.(Picha na Ikulu)

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmaji Mussa Nekela akizunguma na kutowa maelezo kuhusiana na hutuma mbalimbali zinazotolewa na Benki yake kwa Wananchi, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, lililofunguliwa leo 25-7-2022, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiwa katrika ziara yake Pemba.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi wa Wizara ya Afya Zanzibar Said Ali Bakari akitowa maelezo ya michoro ya Hospitali ya Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba inayojengwa kupitia Mradi wa Fedha za Uviko 19, katika eneo la Kinyasini na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh Khamis, akiwa Pemba akiendelea na ziara yake katika Mkoa huo leo 25-7-2022.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisoma jiwe la Msingi la Hospitali ya Wilaya ya Wete Pemba inayojengwa katika Kijiji cha Kinyasini, kupitia Fedha za Uviko -19,baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hospitali hiyo ya Wilaya na (kulia ) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh Khamis, akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba leo 25-7-2022.(Picha na Ikulu) WANANCHI wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akiwahutubia katika hafla ya Ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Wete Pemba leo 25-7-2022.(Picha na Ikulu)

BAADHI ya Waendesha Bodaboda wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akiwahutubia katika hafla ya Ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Wete Pemba leo 25-7-2022.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments