Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimkaribisha Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot leo tarehe 25 Julai, 2022 katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot leo tarehe 25 Jula, 2022, alipomtembelea katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.


Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akikabidhiwa zawadi na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot walipokutana leo tarehe 25 Julai, 2022, katika ofisi ndogo za ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot leo tarehe 25 Julai, 2022, mara baada ya kukutana naye katika ofisi ndogo za ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot pamoja na ujumbe wake leo tarehe 25 Julai, 2022, mara baada ya kukutana naye katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.
**********************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo tarehe 25 Jula, 2022, amekutana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika masuala ya Kazi, Vijana, na Ajira.



Waziri Ndalichako amemuhakikishia Balozi huyo kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana naye na ameomba kuwepo na Programu ya kuwausisha Vijana na masuala ya digitali ili waweze kutumia teknolojia kwa tija.



Naye, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot amesema Uswisi iko tayari kushirikiana na Ofisi hiyo katika kuleta Maendeleo kwa Vijana hususan kupitia Programu zao za Mafunzo ya Uanagenzi.



Viongozi hao wamekutana na kufanya mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo za Ofisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments