Ticker

6/recent/ticker-posts

OKWA ATUMA SALAMA UPANDE WA WAPILI, SIMBA DAY NI KUFURU***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SIMBA DAY, wanamsimbazi leo ni kama ilikuwa siku yao mara baada ya kupokea burudani mbalimbali kutoka kwa wasani, viongozi wao pamoja na wachezaji wao ambao wamezesha mashabiki kumaliza siku ya leo wakiwa na furaha.

Kwanza kabisa mashabiki waliamuakuujaza uwanja wa Benjamini Mkapa ili kuweza kushuhudia burudani kadhaa zikitolewa kwenye uwanja huo.

Wasanii kibao wameweza kutoa burudani mbalimbali kama Zuchu, Tunda Man na wengine kibao ambao wametoa burudani ambayo mashabiki walizipokea kwa shangwe kwenye dimba hilo.

Nje ya burudani hizo kulikuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya St.George ya nchini Ethiopia na kuwafanya Simba Sc kutoka kifua mbele kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Wachezaji wapya ambao wametambulishwa leo hii wameonesha viwango ambavyo mashabiki walitarajia, wachezaji hao ni kama Nelson Okwa ambaye alifunga kwenye mchezo huo,

Post a Comment

0 Comments