Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AHIMIZA WANANCHI KUWEKEZA KATIKA KILIMO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilayani Mbarali katika hafla fupi iliyofanyika Ubaruku, Rujewa Mkoani Mbeya tarehe 08 Agosti, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Ubaruku, Mbarali mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya tarehe 08 Agosti, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Halali Wilaya ya Wanging’ombe alipowasili Mkoani Njombe kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 08 Agosti, 2022.

**************************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameuagiza kila mkoa kutenga eneo litakalotumika kwa kilimo cha mazao yanayozalishwa katika mkoa husika.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) iliyofanyika katika uwanja wa John Mwakangale.

Aidha, Rais Samia amewataka wakulima kutumia maeneo hayo yatakayotengwa kuzalisha kibiashara ili kupata chakula cha kutosha na kuuza kwa nchi jirani.

Vile vile, Rais Samia amewataka wakulima kujisajili ili kupata vitambulisho ambavyo vitatumika kupata ruzuku ya mbolea kuendana na misimu.

Rais Samia pia amemuelekeza Waziri wa Mifugo na Uvuvi kushirikiana na Chuo cha Kilimo (SUA) ili kuwezesha vijana wanaohitimu chuoni hapo kuweza kujiajiri katika sekta hiyo.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameitaka Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa NARCO kufanya uchambuzi wa vitalu vya ranchi vilivyokodishwa na kujua mapato yatokanayo na vitalu hivyo.

Halikadhalika, Rais Samia ameiagiza Wizari ya Mifugo na Uvuvi kufuta leseni za vitalu vilivyokodishwa na kupanga upya ili kufanya uwekezaji wenye tija.

Post a Comment

0 Comments