Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT.MPANGO AWATAKA VIONGOZI SHIMMUTA KUHAKIKISHA WANATENGA FEDHA KURUHUSU WATUMISHI KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pauline Gekul wakati alipowasili katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga kuzindua mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) leo tarehe 20 Novemba 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea maandamano ya timu washiriki wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo inayofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. (Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba na kulia ni Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pauline Gekul) Tarehe 20 Novemba 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi pamoja na washiriki wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo inayofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Tarehe 20 Novemba 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa mwamuzi wa mchezo wa kamba baina ya timu ya TPDC NA TPA wakati akizindua mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) yanayofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Tarehe 20 Novemba 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirikisho la Michezo ya Mashirika Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) mara baada ya uzinduzi wa michuano hiyo inayofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Tarehe 20 Novemba 2022.

********************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewataka viongozi wa Taasisi, Mashirika na Makampuni wanachama wa SHIMMUTA kuhakikisha wanatenga fedha kila mwaka na kuwaruhusu watumishi wao kushiriki michezo hiyo na kutoa kipaumbele kama majukumu mengine muhimu ya kiofisi.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) yanayofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga leo tarehe 20 Novemba 2022.

Pia amewasihi viongozi wa Taasisi, Mashirika na Makampuni Binafsi kuwaruhusu viongozi wa Kamati Tendaji ya SHIMMUTA washiriki kwenye vikao vya uongozi kila inapohitajika kwa maslahi mapana ya wafanyakazi na Taasisi hizo.

Makamu wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi katika sehemu za kazi na watanzania kwa ujumla, kushiriki kwenye michezo, ili kuwa na nguvukazi yenye afya ya mwili na akili ambayo italeta matokeo chanya ya utendaji katika taasisi na kwa maendeleo ya Taifa.

Amesema tafiti zinaonesha kuwa michezo ina faida kwa afya ya mwili na akili hivyo husaidia kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari na shinikizo la damu.

Aidha ametoa wito kwa Taasisi, Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi kuhakikisha wanafanya usafi, kupanda miti na maua katika maeneo yao ya kazi.

Pamoja na kuendelea kushirikiana na Serikali kudhamini Programu mbalimbali zinazohusiana na maendeleo endelevu na utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pauline Gekul amekemea vitendo vya taasisi kushirikisha wanamichezo wasiohusika katika michuano hiyo.

Aidha ameagiza Baraza la Michezo la Taifa kufuatilia taasisi 50 ambazo hazijashiriki katika michuano hiyo kwa miaka miwili mfululizo.

Awali akisoma Risala ya Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Mashirika Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) Roselyne Massam amesema mashindano hayo yameendelea kuwa na mafanikio ambapo kwa mwaka huu zimefika timu 52 kulinganisha na timu 26 mwaka 2018.

Amesema changamoto zinazokabili shirikisho hilo ni pamoja na wanachama kutolipa ada kwa wakati na hivyo kukwamisha shughuli za shirikisho.

Post a Comment

0 Comments