Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT.HUSSEIN MWINYI ASHUHUDIA UTIAJI WA SAINI YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE PEMBA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia Utiaji wa Saini ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba, kati ya Kampuni ya Propav kutoka Nchini Brazil pamoja na Kampuni ya MEECO ya Tanzania na Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, (kulia ) Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Bi.Khadija Khamis Rajab akisaini kwa niaba ya Wizara na Bw. Leondro Motta akisaini kwa niaba ya Kampuni ya Propav ya Brazil,hafla hiyo iliyofanyika leo 4-1-2023, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia Utiaji wa Saini ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba, kati ya Kampuni ya Propav kutoka Nchini Brazil pamoja na Kampuni ya MEECO ya Tanzania na Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, (kulia ) Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Bi.Khadija Khamis Rajab na Mwakilishi wa Kampuni ya Propav ya Brazil .Bwa.Leandro Motta, wakionesha Hati za Makubaliano ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba baada ya kusaini leo 4-1-2023, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza baada ya Utiaji wa Saini ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba, hafla hiyo ya utiaji wa saini kati ya Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar na Kampuni ya Propav kutoka Nchini Brazil, pamoja na MECCO ya Tanzania, iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 4-1-2023.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya Utiaji wa Saini wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba, kati ya Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar na Uongozi wa Kampuni ya Propav kutoka Nchini Brazil pamoja na Kampuni ya MECCO ya Tanzania, hafla hiyo iliyofanyika leo 4-1-2023,katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kubadilishana mawazo na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania David William Concar, baada ya kumalizika kwa utiaji wa Saini ya Ujenzi wa Uwanja mpya wa Ndege Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 4-1-2023.(Picha na Ikulu) WAKUU wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakishuhudia utiaji wa Saini ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 4-1-2023, kati ya Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar na Kampuni ya Propav kutoka Nchini Brazil na Kampuni ya Mecco ya Tanzania.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments