Ticker

6/recent/ticker-posts

TANESCO YAZINDUA MPANGO WA MIAKA MINNE WA KIJINSIA


NAIBU Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia kuanzia mwaka 2023-2027, wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia hafla iliyofanyika leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia hafla iliyofanyika leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.





NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Athuman Selemani Mbuttuka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia hafla iliyofanyika leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.


MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Balozi Mwanaidi Maajar,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia hafla iliyofanyika leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.


MKURUGENZI Mtendaji wa TANESCO,Bw.Maharage Chande ,akielezea malengo yaprogramu hiyo wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia hafla iliyofanyika leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.


SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia kuanzia mwaka 2023-2027, wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia hafla iliyofanyika leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.


NAIBU Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia kuanzia mwaka 2023-2027, wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia hafla iliyofanyika leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.


NAIBU Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato,akizindua logo itakayotumiaka katika Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia kuanzia mwaka 2023-2027, wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia iliyozinduliwa leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.


NAIBU Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia kuanzia mwaka 2023-2027, wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia hafla iliyofanyika leo Machi 30,2023 jijini Dodoma.



Na.Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limezindua Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia kuanzia mwaka 2023-2027, wenye lengo la kuboresha mfumo wa upatikanaji wa takwimu za kijinsia.

Akizindua program hiyo leo Machi 30,2023 jijini Dodoma Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato amesema mradi huo unalenga kutengeneza sera za shirika na kujenga uwezo kuhusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia.

Mhe.Byabato amesema kuwa mradi huu utaenda kuleta usawa wa kijinsia TANESCO kwasababu kutakuwa na mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kujenga uelewa kuwa na uweledi katika masuala ya kinjisia.

“Mradi huu unatekelezwa na TANESCO lengo ni kuhakikisha watumishi wanaofanya kazi katika taasisi hiyo wanapata haki sawa,lengo ni kuhakikisha nafasi mbalimbali zinazojitokeza zinahusisha jinsia zote bila ubaguzi na kujenga usawa.''amesema Mhe.Byabato

Aidha amesema kuwa mradi huo, utasaidia kuwepo kwa taarifa sahihi za unyanyasaji wa kijinsia katika shirika, kuruhusu fursa ya ukuzaji taaluma kwa wafanyakazi wanawake na kuongeza mafunzo kwa vitendo kwa wafanyakazi wanawake waliopo kazini.

”Katika mradi huo tumekubaliana kuunda kitengo maalumu ambacho kitakuwa na bajeti na kujengewa uwezo kuhusu masuala ya jinsia ili mtu anapopata changamoto awe na sehemu ya kwenda kusema na kupata msaada.''ameongeza

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Balozi Mwanaidi Maajar amesema kuwa maendeleo hayawezi kuwepo kama hakutakuwa na usawa wa kijinsia.

“Tunataka wanawake wa TANESCO wawe na haki na wajibu sawa na wanaume kusiwepo na vitendo vya vitisho akashindwa kufanya maamuzi mbalimbali.pia katika meza ya maamuzi na wanawake nao washirikishwe ili kujenga usawa mahali pa kazi.''ameeleza Balozi Maajar

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,Bw.Maharage Chande amesema kuwa lengo la programu hiyo ni kutatua changamoto wanazokutana nazo wanafunzi wanawake katika maeneo yao ya kazi kwa lengo la kukuza ajira zao ili kuongeza idadi ya wanawake wanaoajiriwa.

Amesema maeneo ya kimkakati yatakayopewa kipaumbele kuwa ni kuiboresha sera ya Shirika na kujenga uwezo ili sera iende sambamba na masuala ya kijinsia,kuwepo na taarifa sahihi zinazohusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye Taasisi,kuruhusu fursa ya ukuzaji wa taaluma kwa wafanyakazi wanawake hasa wanaofanyakazi kwenye miradi na kuwepo kwa nafasi ya mafunzo kwa vitengo kwa wafanyakazi wanawake waliopo kazini ili kuwajengea uwezo kuelekea kwenye ajira kamili.

Amesema mradi wa kusafirisha umeme wa Tanzania hadi Zambia (TAZA),Chande ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO wanatekeleza ujenzi wa mradi wa upanuzi wa njia ya kusafirisha umeme mkubwa wa kilovoti 400 kutoka katika kituo cha kupokea,Kupoza na kusafirisha umeme mkubwa cha Tagamenda Iringa kwenda kwenye nchi zilizopo kusini mwa Tanzania(Southern African Power Pool)kupitia Kisada Iringa,Iganjo Mbeya na Nkangamo Tunduma Songwe.

"Mradi huu unafadhiliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Maendeleo (IDA) ya Benki ya Dunia kwa mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 455,Mfuko wa Maendeleo wa Ufaransa (AfD) kwa mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 115,umoja wa Nchi za Ulaya(EU)kwa Dola za Kimarekani milioni 30 pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Dola za Kimarekani milioni 10,"ameeleza

Aidha amekitaja kituo hicho cha Tagamenda kuwa ni kitovu cha kusafirisha umeme mkubwa wa kilovoti 220 kwenda kwenye mikoa takribani 18 nchini.

"Na kwa upande mwingine kituo hiki kimeunganishwa na kituo cha umeme cha zuzu Dodoma ili kusafirisha umeme mkubwa kwenda kwenye nchi zilizopo Mashariki mwa Tanzania ambazo ni Kenya,Uganda na Ethiopia kupitia mradi wa kuunganisha umeme baina ya Kenya na Tanzania(Kenya-Tanzania Power Interconnection Project-KTPIP)

Post a Comment

0 Comments