Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NCHEMBA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisaini kitabu cha Wageni katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, ambako anafanya ziara ya kikazi kwa ajili ya majadiliano na Viongozi wa Taasisi za Kimataifa na baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza kwa ajili ya Mipango ya maendeleo ya Tanzania.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (katikati) akingalia jambo kuhusu miundombinu yaJengo la Ubalozi, kwenye simu ya Mwambata wa Kijeshi- Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Brigedia Jenerali Bright Msuya (kushoto). Kulia ni Balozi wa Tanzania- Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro, wakati mstari wa nyuma, kushoto ni Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justine, Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Rished Bade na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mali za Serikali Bw. Chotto Sendo, Jijini London nchini Uingereza
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania pamoja na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ambako anafanya ziara ya kikazi. Kushoto kwa Mhe. Waziri ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil, Mwambata Fedha, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bi. Anath Lwenduru, na kulia kwake ni Balozi wa Tanzania- Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justine.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, London,Uingereza)

Post a Comment

0 Comments