Ticker

6/recent/ticker-posts

JUMUIYA YA WAZAZI KIBAHA MJI YAWAFUTA MACHOZI WALIOJIFUNGUA KITUO CHA AFYA MKOANINa Victor Masangu,Kibaha


Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya Kibaha mji katika kuboresha afya ya mama na mtoto imeamua kufanya ziara katika kituo cha afya mkoani kilichopo Wilaya ya Kibaha na kufanya matendo ya huruma katika wodi ya wazazi kwa kugawa msaada wa vifaa mbali mbali na mahitaji muhimu.


Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya wazazi Yahaya Mtonda amesema kwamba wameamua kufanya ziara hiyo ya kutembelea kituo hicho cha afya ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya wazazi hivyo wakaona kuna umuhimu kufanya matukio ya kuisaidia jamii.


Mwenyekiti huyo ya wazazi ambaye aliambatana na viongozi mbali mbali wa jumuiya hiyo wakiwemo wajumbe wa kamati ya utekelezaji sambamba na baadhi ya madiwani ambapo walipokelewa kwa furaha na kuweza kupata fursa ya kuwatembelea wazazi waliojifungua kwa ajili ya kuwajulia hali na kuwapatia mahitaji yao muhimu wanayostahili.


Mtonda alisema kwamba jumuiya yao ya wazazi imeona kuna changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wakinamama wajawazito pindi wanapojifungua wanahitaji mahitaji mbali mbali ili kuweza kuwasaidia pindi wanapokuwa wodini wao pamoja na watoto ambao wamezaliwa.

"Tupo katika kipindi cha maadhimisho wiki ya wazazi ambapo kwa Upande wetu kama Wilaya ya Kibaha mji tumeamua kuchagua baadhi ya maeneo kwa ajili ya kuyatembelea ikiwemo kituo Cha afya mkoani hususan katika wodi ya wazazi na tumetoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo sabuni,pampasi za watoto pamoja na mahitaji mengine muhimu kwa ajili ya watoto na wakinamama.


Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kubadilika kwa kuhakikisha kwamba wanawalea na kuwatunza watoto wao kwa lengo la kuijenga nchi na kwamba wataendelea kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazokikabili kituo hicho ikiwemo kuboresha miundombinu ya majengo ili wagonjwa waweze kupata huduma nzuri.

Awali mganga mfawadhi wa kituo cha afya Mkoani Abdulkadri Sultan ameipongeza kwa dhati jumuiya hiyo ya wazazi kutokana na kuona umuhimu mkubwa wa kutumia wiki ya maadhimisho yao kwenda kutoa msaada katika wodi ya wazazi kwani wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mahitaji pindi wanapojifungua.


Sultan alisema kuwa licha ya jumuiya ya wazazi kwenda kutoa msaada lakini kwa Sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kupokea idadi kubwa ya wagonjwa ukilinganisha na idadi ya wodi zilizopo ni chache hivyo kuiomba jumuiya hiyo iwasadie katika jambo hilo.


Naye diwani wa Kata ya Tumbi ambaye naye alishiriki katika ziara hiyo hakusita kuwashukuru kwa dhati uongozi mzima wa jumuiya ya wazazi Wiyala ya Kibaha mji kwa kuona umuhimu wa kuwasapoti kwa hali na mali wakinama hao pamoja na watoto wao.


Nao baadhi wa wakinamama ambao walipata fursa ya kutembelewa na kupatiwa msaada wa vitu mbali mbali wamesema kitendo hicho kimeweza kuwafariji kwa kiasi kikubwa kwani hawakuweza kutegemea kama watapatiwa msaada huo kwani utawasaidi wao pamoja na watoto wao.


Katika hatua nyingine uongozi wa jumuiya hiyo uliweza kutoa salamu zao kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka pamoja na mke wa Mbunge Selina Koka kwa kuweza kusapoti kufanikisha zoezi hilo pamoja na wadau wengine wakiwemo baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji Kibaha.Post a Comment

0 Comments