Ticker

6/recent/ticker-posts

UGAWAJI MAENEO YA BIASHARA SOKO LA KARIAKOO KUWA LA UWAZI- GHASIA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia ( wa kwanza kulia) akikagua ukarabati wa soko la zamani la Kariakoo linaloendelea kujengwa na serikali jijini Dar es Salaam ambapo limefikia asilimia 71 leo Aprili 12,2023

*********************

Na. KMC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Hawa Abdulrahman Ghasia amesema bodi hiyo imejipanga kuhakikisha mradi wa ukarabati na ujenzi wa soko la Kariakoo utakamilika ndani ya muda wa mkataba na kwa ubora ambapo ugawaji wa maeneo ya biashara utakuwa wa uwazi.

Akiwa kwenye eneo la mradi huo leo Aprili 12,2023 jijini Dar es Salaam ,Ghasia ameelezea kuridhishwa kwake na kazi inayoendelea kufanywa na mkandarasi kampuni ya ESTIM construction Ltd ambapo serikali ya awamu ya sita imetoa shilingi Bilioni 28.03.

Akizungumzia kuhusu mchakato wa ufanyaji biashara mara baada ya mradi kukamilika, Ghasia alisema ugawaji wa maeneo ya kufanyia biashara ikiwemo maduka na vizimba utakuwa wa wazi na kwamba wananchi watapatiwa taarifa rasmi .

"Mchakato wa ugawaji maduka ,vizimba na meneo mengine ya biashara utafanyika kwa uwazi ili kila mwananchi mwenye sifa apate eneo la biashara " alisema Ghasia.

Serikali ilianza kutekeleza mradi huo wa ukarabati wa soko la zamani lililoungua na ujenzi wa soko jipya la Karikaoo Januari 2022 na utakamilika Oktoba 2023 ambapo Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) ni Mshauri Elekezi na ujenzi ukifanywa na kampuni ya ESTIM Contraction Company Ltd ambapo hadi Machi mwaka huu mradi umefikia asilimia 71.

Post a Comment

0 Comments