Ticker

6/recent/ticker-posts

IGP WAMBURA AONGOZA KIKAO CHA KUPIMA UTENDAJI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura, Mei 25, 2023 aliongoza kikao cha 15 cha kupima utendaji kazi kilichohusisha Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Polisi, Makamanda wa Polisi wa Vikosi na Vyuo Jijini Dodoma.

Ambapo Katika kikao hicho wamejadili mafanikio yaliyopatikana, changamoto kwa kipindi kilichopita, muono mbele na kuweka mikakati ya kutekeleza majukumu ya Jeshi la Polisi kwa ufanisi zaidi katika kubaini,kuzuia na kutanzua uhalifu.

Vikao vya aina hii hufanyika mara nne kwa mwaka. Picha na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi.

Post a Comment

0 Comments