Ticker

6/recent/ticker-posts

PIKIPIKI 85 ZAKABIDHIWA KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NCHINI


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa Pikipiki kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata 85 nchini iliyofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa Pikipiki kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata 85 nchini iliyofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi (Elimu), Dk Charles Msonde,akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa Pikipiki kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata 85 nchini iliyofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bw. Amon Mpanju,akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa Pikipiki kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata 85 nchini iliyofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa Pikipiki kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata 85 nchini iliyofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Pikipiki kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata 85 nchini iliyofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.

PICHA ZOTE NA ALEX SONNA


SERIKALI imegawa jumla ya pikipiki 85 kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata 85 nchini ili kuwezesha utekekezaji wa majukumu yao.

Akikabidhi pikipiki hizo zitakazokwenda kwenye mikoa 21 Halmashauri 47 na kata 85 nchini, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali inafanya jitihada kuweka mazingira wezeshi ya utendaji kazi wa Maafisa Maendeleo ya Jamii waliopo huku ikiendelea kushughulikia changamoto ya upungufu wao.

Dkt. Gwajima amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ajira 800 za Maafisa Maendeleo ya Jamii ambazo zitapunguza kwa kiasi kikubwa uhaba uliopo.

"Jitihada hizi zote zinazofanywa na Serikali kwa lengo la kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi, hususan wanawake ambao katika kipindi cha nyuma walisahauliwa katika elimu na mipango ya maendeleo hivyo kuwanyima fursa ya kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Nchi yetu" amesema Dkt. Gwajima.

Aidha, Dkt. Gwajima ameongeza kuwa, Maafisa Maendeleo ya Jamii wamekuwa ni kiunganishi kikuu katika Jamii kati Wanawake na fursa za mikopo pamoja na wataalamu wa fani mbalimbali kwenye upatikanaji wa teknolojia sahihi za uzalishaji, uchakataji, masoko na vifungashio kwa Wanawake Wajasiriamali.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bw. Amon Mpanju,amesema kuwa lengo la Wizara kushirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kununua pikipiki hizo zenye thamani ya sh. milioni 314 ni kuhakikisha Maafisa Maendeleo ya Jamii wanaamsha na kuchechemua ari ya maendeleo, kubainisha fursa zilizopo ndani ya jamii na kuhimiza kuzitumia.

Mpanju amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kuhimiza masuala ya maendeleo ngazi ya msingi, kuwawezesha Maafisa Maendeleo ya Jamii kurahisisha majukumu yao na kuiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI kufanya mgao kwaku zingatia mahitaji halisi.

"Vigezo tulivyotumia ni kugawa pikipiki hizi kwenye mikoa yenye inayoongoza kwa vitendo vingi vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kata zilizopo pembezoni na maeneo yenye Maafis Maendeleo ya Jamii wachache zaidi" ameongeza Mpanju.

Naye ANaibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amebainisha kuwa changamoto mojawapo ya Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na uhaba ni usafiri ambapo kwa juhudi za Halmashauri hadi sasa zilizopo ni pikipiki 77 pekee.

Ameongeza kwamba, anatambua juhudi za pamoja za Serikali na mageuzi makubwa hasa mapango wa taifa wa kusimamia maendeleo ngazi yamsingi.

"Wananchi ndio wawe kitovu cha kuleta maendeleo kwa kuibua, kupanga na kufuatilia maendeleo yao hivyo wanahitaji mageuzi mapya kifkra" amesema Dkt. Msonde.

Dkt. Msonde amempongeza Waziri Dkt. Gwajima na Wizara anayoiongoza kwa jitihada wanazochukua kuhakikisha pikipiki hizo 85 zinapatikana.

Post a Comment

0 Comments