Ticker

6/recent/ticker-posts

KINANA AKUTANA NA KIONGOZI WA NATIONAL DEMOCRATIC INSTITUTE YA MAREKANI.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdulrahman Kinana, leo Agosti 24, 2023, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa taasisi ya Marekani ya NDI inayojishughulisha na masuala ya demokrasia, Balozi Derek Mitchel, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.

Balozi Mitchel ameipongeza serikali ya CCM kwa hatua nzuri iliyopigwa katika kukuza demokrasia nchini Tanzania.

Makamu Mwenyekiti Ndugu Kinana amemhakikishia kiongozi huyo kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania itaendelea kufanya mageuzi yatakayoimarisha demokrasia nchini.


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdulrahman Kinana, leo Agosti 24, 2023, Akizungumza na Rais wa taasisi ya Marekani ya NDI inayojishughulisha na masuala ya demokrasia, Balozi Derek Mitchel, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam. (Picha na Fahadi Siraji)


Post a Comment

0 Comments