Ticker

6/recent/ticker-posts

TTCL YAFIKISHA HUDUMA YA FAIBA KATIKA JENGO JIPYA LA MAKAO MAKUU YA PAPU JIJINI ARUSHA

Waziri wa Mawasiliano nchini Afrika Kusini Bw. MONDLI GUNGUBELE (kushoto) akipeana mkono na Meneja wa TTCL Mkoa wa Arusha Bw. FREDRICK MLOKA (kulia) wakati alipotembelea Banda la TTCL kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati wa Kikao cha 41 cha Baraza la Umoja wa Posta Afrika kinachofanyika jijini Arusha
Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akimwelezea Waziri wa Posta na Mawasiliano wa Liberia Bw. WORLEA SAYWAH DUWAH huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inayosimamiwa na kuendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 41wa Baraza la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) wametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nakuoneshwa miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano inayosimamiwa na shirika hilo.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 41wa Baraza la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) wametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nakuoneshwa miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano inayosimamiwa na shirika hilo.


Na Mwandishi wetu Arusha

Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL ni miongoni mwanTaasisi na Mashirika ya Umma yaliyochini ya Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yanayoshiriki maonesho yaliyoandaliwa na Wizara hiyo wakati wa Kikao cha 41 cha Baraza la Umoja wa Posta Afrika kinachofanyika jijini Arusha.

Meneja Biashara ambaye pia ni Meneja wa Banda katika maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) Bw. Laibu Leonard amesema moja kati ya faida ya kushiriki Maonesho hayo ni kuendelea kuifungua nchi katika sekta ya utalii kwani TTCL inaonesha matukio ya moja kwa moja yanayoendelea katika mlima kilimanjaro.

Bw. Leonard amesema kupitia maonesho hayo nchi 30 kati ya nchi wanachama 45 wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) zimenufaika na kasi ya mtandao iliyotolewa na TTCL na hivyo kuziwezesha kufanikisha matukio mbalimbali yanayohusu ajenda za Kikao hicho.


AmesemaTTCL imebeba dhamana ya kuhakikisha washiriki wote wanapata mtandao wa uhakika na kasi ili dhamira ya kikao hicho ya kufanya shughuli za Posta kufanyika kidigitali iweze kuonekana inatekelezeka.

"Shirika letu tunawaunganishia washiriki wote hapa Wireless ya bure yenye kasi ya 10G no mtandao wa uhakika na haukwamikwami na hapa pia tunaonesha Moja kwa moja matukio yanayoendelea katika mlima Kilimanjaro kwanzia mwanzo mpaka Uhuru peak" amesema Laibu

Ameongeza kuwa kupitia maonesho ya Banda la TTCL ni wazi watavutiwa na upo uwezekano kwa baadhi wakimaliza Mkutano wanaweza kwenda kutembelea mlima huo ili kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Hifadhi ya mlima Kilanjaro.

Aidha amesemaNa Kupitia Mkutano huu wa PAPU Shirika (TTCL ) limepata fursa ya kuonyesha huduma zake kwa wageni ambapo huduma hizo ni pamoja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) huduma za Data Center (NIDC) hivyo washiriki wameweza kupata uelewa wa namna miradi hii ya kimkakati inavyosamiwa na umuhimu wake kwa Wananchi.

Aidha, Bw. Leonard amesema kuwa maonesho haya yanafanyika kuelekea Siku ya Uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) utakaofanyika Septemba 2 Mwaka huu ambapo mpaka sasa TTCL wameshafikisha huduma ya Faiba katika Jengo hilo ili kuhakikisha shughuli zote za kiposta zinatekelezeka kidigitali.

Pia Leonard ameongeza kuwa Shirika hilo kama msimamizi na mwendeshaji wa miradi ya mawasiliano ya kimkakati linatekeleza majukumu yake ya kuhakikisha miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inajengwa nchini hadi nje ya mipaka ya Tanzania ili kuziwesha shughuli za Posta ndani na nje ya Afrika kufanyika vizuri.

Post a Comment

0 Comments