Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI WA FEDHA NA WAZIRI WA KILIMO WATETA NA UJUMBE WA NMS INFRASTRUCTURE

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza kuhusu umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya kilimo wakati wa mkutano na ujumbe kutoka  Kampuni ya NMS Infrastructure kutoka nchini Uingereza, ikiongozwa na Mratibu wa Kampuni hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki, Bw. Tom Vaughan (hayupo pichani), jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, akizungumza jambo kuhusu mpango wa Serikali wa kuongeza nguvu ya uwekezaji katika sekta ya kilimo hususan katika kuongeza uzalishaji na mnyororo wa thamani katika mazao ya kilimo, wakati wa mkutano na ujumbe wa Kampuni ya NMS Infrastructure ya nchini Uingereza,  ikiongozwa na Mratibu wa Kampuni hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki, Bw. Tom Vaughan (hayupo pichani), jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, wakisikiliza kwa makini wasilisho la Kampuni ya NMS Infrastructure ya nchini Uingereza, kutoka kwa Mratibu wa Kampuni hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki, Bw. Tom Vaughan (hayupo pichani), kwenye mkutano wa Ujumbe wa Kampuni hiyo na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), jijini Dodoma. 
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, akizungumza jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) na Ujumbe wa Kampuni ya NMS Infrastructure ya Uingereza, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) wakiwa katika mkutano na Ujumbe wa Kampuni ya NMS Infrastructure ya Uingereza, ulioangazia uwekezaji kwenye sekta ya kilimo, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma) 

Post a Comment

0 Comments