Ticker

6/recent/ticker-posts

TISEZA YAZINDUA DAWATI LA HUDUMA KWA WAWEKEZAJI SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, na Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TISEZA, Bw. Felix John (kulia), wakikabidhiana nyaraka za kuscan (QR Codes) wakati wa uzinduzi wa Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga.  

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imezindua rasmi Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga, hatua inayolenga kusogeza huduma za uwekezaji karibu zaidi na wananchi, hususan wawekezaji wa ndani na wajasiriamali wa mkoa huo.

Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa, Januari 30, 2026, sambamba na utekelezaji wa semina ya uhamasishaji wa uwekezaji wa ndani iliyowakutanisha wajasiriamali, wafanyabiashara, wawekezaji na wadau mbalimbali wa sekta ya uwekezaji mkoani Shinyanga. 

Tukio hilo ni sehemu ya Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji wa Uwekezaji wa Ndani inayoendelea kutekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita.

Katika hatua ya kuimarisha utekelezaji wa dawati hilo, TISEZA imekabidhi nyenzo muhimu za kazi kwa ajili ya kuanza rasmi kutoa huduma, huku Dawati hilo likitarajiwa kufanya kazi ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ili kurahisisha uratibu na utoaji wa huduma kwa wawekezaji.

Akifungua semina hiyo na kuzindua Dawati la Huduma kwa Wawekezaji, Mhe. Mboni Mhita amewahimiza Watanzania, hususan wawekezaji wa ndani, kuchangamkia fursa lukuki za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga, akisisitiza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko tayari kushirikiana kwa karibu na wawekezaji wote katika kufanikisha miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita.

Mhe. Mhita amepongeza juhudi za TISEZA katika kutekeleza mikakati ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani, akibainisha kuwa Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuhakikisha wawekezaji wanapata huduma stahiki, mazingira rafiki ya biashara na uhakika katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Shinyanga umejipanga kikamilifu kupokea uwekezaji mkubwa zaidi kupitia maeneo maalum yaliyotengwa rasmi kwa ajili ya uwekezaji, sambamba na kuendelea kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kujitokeza kuwekeza katika sekta mbalimbali za kiuchumi zenye tija.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TISEZA, Bw. Felix John, amesema Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Shinyanga litakuwa na jukumu la kuwahudumia wawekezaji kwa karibu na kwa haraka, kutoa taarifa sahihi za uwekezaji, kuratibu masuala ya usajili wa miradi, pamoja na kusaidia utatuzi wa changamoto zinazoweza kujitokeza kwa wawekezaji waliopo mkoani humo.
Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TISEZA, Bw. Felix John.

“Leo tumezindua rasmi Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuleta huduma za uwekezaji karibu na wananchi, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa Novemba 14, 2025, wakati akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema John.

Ameeleza kuwa utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji wa Uwekezaji wa Ndani ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2025–2030, sambamba na adhima ya Rais Samia ya kuifungua nchi kwa wawekezaji wa ndani na nje.

John amesema lengo kuu la kampeni hiyo ni kubadili mtazamo na fikra za Watanzania kuhusu uwekezaji, akieleza kuwa kwa muda mrefu dhana ya uwekezaji imekuwa ikihusishwa zaidi na wawekezaji wa kigeni, huku Watanzania wengi wakijiona kama watazamaji badala ya wahusika wakuu.

“Kupitia kampeni hii tunawahamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika nchi yao wenyewe. Mojawapo ya mikakati yetu ni kutoa elimu ya uwekezaji kupitia semina kama hii, hususan kwa wananchi wa mikoa husika, ikiwemo Shinyanga,” ameongeza.

Amebainisha pia kuwa TISEZA, wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga, imepata fursa ya kutembelea miradi ya wawekezaji wa ndani waliothubutu kusajili miradi yao kupitia TISEZA, na kunufaika na vivutio mbalimbali vya kikodi na visivyo vya kikodi, hali iliyowasaidia kupunguza gharama za mtaji na kuimarisha utekelezaji wa miradi yao.

“Tunatarajia baada ya semina hii, idadi ya wawekezaji wa ndani mkoani Shinyanga itaongezeka kwa kiasi kikubwa, jambo litakalochangia ukuaji wa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla,” amesema John.
Katika semina hiyo, Bw. Felix John amewasilisha mada ya kina iliyogusia fursa mbalimbali za uwekezaji, sekta za kipaumbele, vivutio vinavyotolewa na Serikali, pamoja na taratibu na mchakato wa usajili wa miradi ya uwekezaji kupitia TISEZA.

Washiriki wa semina hiyo wamepata fursa ya kujadili hoja mbalimbali, kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu mazingira ya uwekezaji nchini na huduma zinazotolewa na TISEZA, hatua iliyosaidia kuongeza uelewa na hamasa ya uwekezaji wa ndani.

Kupitia semina hiyo na uzinduzi wa Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga, TISEZA imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya dhati ya kusogeza huduma za uwekezaji karibu na wananchi, kwa lengo la kuongeza ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji na kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, na Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TISEZA, Bw. Felix John (kulia), wakikabidhiana nyaraka za kuscan (QR Codes) wakati wa uzinduzi wa Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TISEZA, Bw. Felix John (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita nyaraka wakati wa uzinduzi wa Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga na ufunguzi wa semina ya uhamasishaji wa uwekezaji wa ndani 

Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TISEZA, Bw. Felix John akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga na ufunguzi wa semina ya uhamasishaji wa uwekezaji wa ndani 

Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TISEZA, Bw. Felix John akiwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji, sekta za kipaumbele, vivutio vinavyotolewa na Serikali, pamoja na taratibu na mchakato wa usajili wa miradi ya uwekezaji kupitia TISEZA.

Post a Comment

0 Comments